Nenda kwa yaliyomo

Asia Alfasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Asia Alfasi (amezaliwa 20 Aprili 1984) ni msanii na mwandishi wa vichekesho (comic artist) mwenye asili ya Libya na Uingereza, anayejulikana kwa kazi zake zinazoathiriwa na mtindo wa manga. Alizaliwa Libya na alihamia Uskoti akiwa na umri wa miaka saba. Kwa sasa anaishi Birmingham, Uingereza.[1]

Kazi za Alfasi huonyesha mchanganyiko wa ushawishi wa Uislamu, utamaduni wa Kilibya, utamaduni wa Kiingereza, na sanaa ya Kijapani. Alianza kujulikana zaidi baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kushiriki na pia kushinda shindano la Hi8us Midlands Stripsearch, akishinda kupitia mkusanyiko wa kazi zake uliomwonyesha mhusika wake Monir.[2]

  1. "Platform for art – Thin Cities – Asia Alfasi". Transport for London. Desemba 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Februari 2007. Iliwekwa mnamo 23 Desemba 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "BBC - Birmingham - Features - Manga champ". www.bbc.co.uk. Iliwekwa mnamo 2024-12-23.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Asia Alfasi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.