Nenda kwa yaliyomo

Asi Archibong-Arikpo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Asi Archibong-Arikpo (Novemba 12, 1919 – Novemba 22, 2005) alikuwa mkunga, mwanasiasa, na mbunifu wa mitindo wa nchini Nigeria.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Asi Archibong alizaliwa huko Calabar, na wazazi wake William Archibong Young na Umo Archibong Young, wenye asili ya kabila la Efik. Alisoma elimu ya sekondari katika shule ya Duke Town Presbyterian huko Calabar, na kupata mafunzo ya Ukunga huko Dublin, Ireland.[1]

Archibong-Arikpo alikuwa mkuu wa hospitali ya uzazi huko Ugep, Nigeria, kwa miaka miwili. Archibong-Arikpo pia alipata taaluma ya ubunifu wa mitindo. Mnamo 1963, alisema alikuwa akifanya kazi ya kutayarisha vazi la kitaifa la bibi harusi nchini Nigeria.[2] Gauni zake alizokua akitengeneza mara nyingi zilikuwa za bluu na dhahabu, rangi zilizokuwa zikiendana na Kanisa la Presbyterian. Mauzo ya fedha zilizopatikana zilikua kwa ajili ya msaada katika shughuli za misheni ya kanisa.[1]

  1. 1.0 1.1 William Arikpo, "Hon. Elder (Chief) Mrs. Asi Archibong-Arikpo" Archived 2016-10-19 at the Wayback Machine Nigerian Chronicle (25 August 2015).
  2. Bonnie Seymour, "Too Much Time or Not Enough?" The Fresno Bee (16 November 1963): 7. via Newspapers.comOpen access icon
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Asi Archibong-Arikpo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.