Asha Ismail
Asha Ismail (alizaliwa Garissa, Kenya, 27 Septemba 1968) ni mwaharakati wa haki za binadamu nchini Kenya. Ni mwanzilishi wa shirika la Save a Girl, Save a Generation. Shirika ambalo lengo lake kuu ni kumaliza ukeketaji wa wasichana, mfumo wa utoaji mahari, ndoa za kulazimishwa na dhuluma zozote zile dhidi ya wanawake wa bara la Afrika na la Asia.
Maisha na kazi yake
[hariri | hariri chanzo]Alifanyiwa ukeketaji akiwa na umri wa maiaka 5 kwa kile alichoambiwa kuwa ni sherehe ya kutakaswa na kula.Alipokuwa kwenye hedhi na kipindi cha kumzaa bintiye alipita maumivu makali kutokana na madhara aliyofanyiwa, sababu iliyomfanya kuwa na lengo la kutoa elimu ili kumaliza tamaduni hiyo ili msichana wake na wanawake wengine wasipitie yaliyomfika. [1] [2] Katika kijiji chake, kuna wasichana wanaojulikana kama "wasichana wa Asha" kwa sababu amewaokoa kutokana na ukeketaji. Alihamia nchini Uhispania mnamo mwaka wa 2011, na kuanzisha shirika lisilo la kiserikali la Save a Girl, Save a Generation. [3] [4] Binti yake, Hayat Traspas, pia ni mwanachama wa shirika hilo ambalo makao yake makuu ni mjini Madrid. [2]
Ni mmoja wa wanaharakati ambao taarifa zao zilielezewa kwenye filamu ya La manzana de Eva ("The apple of Eve") na José Manuel Colón mwaka wa 2018.Filamu hiyo inaelezea tarifa za wanawake kutoka mataifa tofauti tofauti duniani wanaoendesha kampeni dhidi ya ukeketwaji wa wasichana [5] Alishirika kwenye kampeni ya ujasiri ya Amnesty International's mwaka wa 2017 inayowatambua wanaharakati wa haki za binadamu. [6]
Utambuzi
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 8 mwezi wa Machi mwaka wa 2017, kwenye sherehe ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Ismail alipokea tuzo ya Atenea de Alcobendas kwa kutetea haki za wanawake. [7]
Tarehe 12 mwezi wa Oktoba mwaka wa 2019,alihudhuria sherehe ya kumbukumbu ya miaka kumi na tano ya NGO ya Tierra de Hombres ambapo alikabidhiwa sanamu iliyotengenezwa na mchongaji sanamu Julia Ares kwa kutambua kazi yake. [8] Pia mwezi wa Oktoba mwaka wa 2019 alipokea tuzo kutoka kwa tamasha la Periplo huko Puerto de la Cruz. [9]
Tarehe 24 mwezi wa Januari mwaka wa 2020, Wakfu wa Kimataifa wa Haki za Kibinadamu ulimzawadi Ismail zawadi ya Nicolás Salmeron Tuzo ya Haki za Kibinadamu katika kitengo cha 'Usawa'. [10]
Siku ya Kimataifa ya Wanawake mwaka wa 2020, alipokea tuzo kutoka kwa Jumuiya ya Madrid ambayo aliikataa kwa kile alichodai kuwa haiendani na kanuni na kazi yake.Alishukuru hatua hiyo ya kutunukiwa tuzo hiyo, lakini akasema Serikali ya Madrid ilikuwa kikwazo katika juhudi za kutetea wanawake na unyanyasaji wa kijinsia. [11]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Romero, Noelia Izquierdo (2021-02-09). "Mutilación genital femenina, "no se limita a un continente o a un color"". EfeSalud (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 2021-10-22.
- 1 2 Moreno, Sonia (2021-03-26). "La huida de Asha a Madrid para salvar a su hija de la ablación: 10.000 niñas en España están en peligro". El Español (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 2021-10-22.
- ↑ admin. "Home". Save a Girl Save a Generation (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2023-10-18.
- ↑ Luna, Victoria (2014-02-06). "Asha Ismail, víctima de ablación: "Me prometí que mi hija no pasaría por esa pesadilla"". www.20minutos.es - Últimas Noticias (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 2021-10-22.
- ↑ "La manzana de Eva". Premios Goya. 2018.
- ↑ "Premio Nicolás Salmerón de Derechos Humanos". Fundación Internacional de Derechos Humanos (kwa Kihispania). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-01-18. Iliwekwa mnamo 2021-10-22.
- ↑ Sánchez Carbonell, Angel (2017-03-09). "Entrega de Premios Atenea y Hombres por la Igualdad de Alcobendas". Cronica Norte (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 2021-10-22.
- ↑ "Gala XV Aniversario Tierra de hombres Galicia | Fundación Tierra de hombres España" (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 2021-10-22.
- ↑ "Periplo galardona a Leonardo Padura, Alfonso Armada, Asha Ismail y José Manuel Peruyera". Excelentísimo Ayuntamiento de Puerto de la Cruz (kwa Kihispania). 2019-10-16. Iliwekwa mnamo 2021-10-22.
- ↑ "Premio Nicolás Salmerón de Derechos Humanos". Fundación Internacional de Derechos Humanos (kwa Kihispania). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-01-18. Iliwekwa mnamo 2021-10-22."Premio Nicolás Salmerón de Derechos Humanos". Fundación Internacional de Derechos Humanos (in Spanish). Archived from the original on 2023-01-18. Retrieved 2021-10-22.
- ↑ Desalambre, Europa Press / (2020-03-06). "La activista contra la mutilación genital Asha Ismail rechaza el reconocimiento de la Comunidad de Madrid por el Día de la Mujer". ElDiario.es (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 2021-10-22.