Asha-Rose Mtengeti Migiro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Asha-Rose Migiro

Asha-Rose Mtengeti Migiro (*1956) aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Amepewa cheo hiki na Katibu Mkuu Ban Ki-moon tar. 5 Januari 2007.

Hadi kuteuliwa kwa cheo cha UM alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania tangu Januari 2006. Wajibu huo alipewa na rais Jakaya Kikwete aliyemteua kumfuata katika wizara ya mambo ya nje iliyoshikwa awali na Kikwete mwenyewe.

Chini ya raisi Benjamin Mkapa Migiro alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Alikuwa mbunge kwa njia ya kiti maalumu cha wanawake.

Kabla ya kujiunga na siasa alifundisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alisoma digrii za bachelor na master Dar es Salaam. Mwaka 1992 akaongeza cheti cha udaktari wa sharia kwenye Chuo kikuu cha Konstanz (Ujerumani). Akarudi Tanzania alipoanza kufundisha. Akawa mwanachama wa CCM

Akiwa Mwislamu ameolewa na Cleophas Migiro wana watoto wawili wa kike.

Kwa sasa Dkt. Asha Rose Migiro ameteuliwa kuwa waziri wa katiba na sheria wa Jamuhuri ya muungano TANZANIA

Viungo vya Nje

Habari za Asha-Rose Mtigiro kwenye tovuti rasmi ya Bunge la Tanzania


Administradors.png Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Asha-Rose Mtengeti Migiro kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Pia ni mke wa dr Ritchie lunyonga.