Nenda kwa yaliyomo

Artemisia Gentileschi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Artemisia Lomi Gentileschi (8 Julai 15931653) alikuwa mchoraji wa Kibaroko kutoka Italia. Gentileschi anachukuliwa kuwa mmoja wa wasanii waliotukuka zaidi wa karne ya 17, na awali alifanya kazi kwa mtindo wa Caravaggio. Alianza kutoa kazi za kitaalamu akiwa na umri wa miaka 15. Katika enzi ambayo wanawake walikuwa na fursa chache za kupata mafunzo ya kisanii au kufanya kazi kama wasanii wa kitaalamu, Gentileschi alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa mwanachama wa Accademia di Arte del Disegno huko Florence, na alikuwa na wateja wa kimataifa. Alifanya kazi kama mchoraji wa uhamishoni katika ikulu ya Charles I wa Uingereza kuanzia mwaka 1638 hadi 1642, lakini inadhaniwa alikimbia nchi wakati wa hatua za mwanzo za Vita ya Kiraia ya Uingereza. Baada ya hapo alitoweka kwa muda, na alionekana tena Naples mwaka 1649. Barua yake ya mwisho inayojulikana, aliyomwandikia mmoja wa walimu wake mwaka 1650, inaonyesha kuwa bado alikuwa akifanya kazi kama msanii. Tarehe ya kifo chake haijulikani kwa uhakika, lakini inadhaniwa kuwa alikuwa miongoni mwa wahanga wa Tauni ya Naples ya mwaka 1656.

Uchoraji wake mwingi ulihusisha wanawake kutoka kwenye hekaya, taswira za kifumbo na Biblia—akiwajumuisha waathirika, waliouawa au wapiganaji. Baadhi ya kazi zake maarufu ni *Susanna and the Elders* (hasa toleo la mwaka 1610 lililo katika Schloss, *Judith Slaying Holofernes* (toleo la 1614–1620 lililoko katika Uffizi, na *Judith and Her Maidservant* (kazi yake ya mwaka 1625 iliyo katika Detroit Institute of Arts.[1][2][3][4] [5]

  1. Locker, Jesse (2015). "Artemisia in the Eyes of the Neapolitan Poets". Artemisia Gentileschi: The Language of Painting. New Haven, Connecticut: Yale University Press. ISBN 978-0300185119.
  2. "Violence and Virtue: Artemisia Gentileschi's Judith Slaying HolofernesKigezo:-"
  3. Artemisia Gentileschi Biography
  4. 10 Facts You May Not Know About Artemisia Gentileschi
  5. Announcement of American Academy of Arts and Letters Award for Artemisia, the opera
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Artemisia Gentileschi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.