Arsinoe III
| Arsinoe III Thea Philopator | |
|---|---|
| Malkia wa Misri | |
| Uso wa sarafu unaomuonyesha Arsinoe III | |
| Amefariki | 204 BC |
| Mwenza | Ptolemy IV |
| Baba | Ptolemy III |
| Mama | Berenice II |
Arsinoe III Philopator alikuwa Malkia wa Misri ya Ptolemaic kuanzia mwaka 220 KK hadi 204 KK. Alikuwa binti wa Ptolemy III na Berenice II, na pia mke wa kaka yake Ptolemy IV, huenda akiwa mtawala mwenza. Ndiye malkia wa kwanza wa kifamilia cha Ptolemaic aliyezaa mtoto na kaka yake.[1]
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Kati ya mwishoni mwa Oktoba na mapema Novemba mwaka 220 KK, aliolewa na kaka yake mdogo, Ptolemy IV. Alishiriki kikamilifu katika utawala wa nchi, angalau kwa kiwango ambacho kilivumiliwa na waziri mwenye nguvu kubwa, Sosibius.[2]
Mwaka 217 KK, alisafiri pamoja na Ptolemy IV akiwa na wanajeshi 55,000 katika Vita vya Raphia huko Palestina dhidi ya Antiochus Mkuu aliyekuwa na wanajeshi 68,000.Huenda Arsinoe aliwahi kuongoza sehemu ya wanajeshi wa miguu wa aina ya phalanx.[3]Pande zote mbili zilitumia wapanda farasi, tembo, na vikosi maalumu kama vile wapiga-mishale, pamoja na askari wa jadi wa phalanx ya Kimasedonia.[3] Wakati vita vilipoanza kwenda vibaya, alijitokeza mbele ya wanajeshi na akawahimiza kupigana ili kuwalinda familia zao. Pia aliahidi kumpa kila mmoja wao dhahabu yenye uzito wa minae mbili endapo wangeshinda vita hivyo hata hivyo ni jambo ambalo walifanikiwa.[4]
Katika majira ya joto ya mwaka 204 KK, Ptolemy IV alifariki. Wapendwa wake wawili wakuu, Agathocles na Sosibius, kwa kuogopa kwamba Arsinoe angechukua utawala wa mlezi hivyo walimfanyia mauaji kupitia Philammon katika mapinduzi ya ikulu [5] kabla hajapata taarifa za kifo cha mumewe na wakajihakikishia wenyewe nafasi ya ulezi wa kifalme.
Alama
[hariri | hariri chanzo]Eratosthenes aliandika maandiko yaliyoitwa Arsinoe, ambayo kwa sasa yamepotea, na mada yake ilikuwa ni kumbukumbu ya malkia huyo. Maandishi hayo yamenukuliwa na wasomi wengi wa kale.[6]
Picha zinazofanana naye pia ni nadra, lakini zipo katika umbo la sanamu ya marumaru, [7]na nyingine ya shaba.[8]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Arsinoe III alikuwa na cheo cha mtawala, lakini hakujumuishwa katika taratibu za upangaji tarehe kama mtawala mwenza wa mumewe, jambo lililofanya hadhi yake kuwa ya kutatanisha. Tara Sewell-Lasater anamuweka katika kundi la malkia-mwenza.Hata hivyo Arsinoe anachukuliwa kuwa Farao na Sally Ann Ashton.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://books.google.co.tz/books?id=VMWIDwAAQBAJ&pg=PT226&redir_esc=y
- ↑ https://books.google.co.tz/books?id=FO_fBgAAQBAJ&pg=PA112&redir_esc=y#v=onepage&q&f=false
- 1 2 https://archive.org/details/chronicleofqueen00tyld/page/194/mode/2up
- ↑ Meyers, Carol; Craven, Tony; Kraemer, Ross S., eds. (2000). Women in Scripture: A Dictionary of Named and Unnamed Women in the Hebrew Bible, the Apocryphal/Deuterocanonical Books, and the New Testament. New York: Houghton Mifflin. p. 397. ISBN 0-395-70936-9.
- ↑ https://www.instonebrewer.com/TyndaleSites/Egypt/ptolemies/arsinoe_iii_fr.htm
- ↑ https://search.worldcat.org/title/1154099146
- ↑ https://egymonuments.gov.eg/en/collections/marble-bust-of-arsinoe-iii-9/
- ↑ https://www.getty.edu/publications/artistryinbronze/large-scale-bronzes/5-butz/
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Arsinoe III kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |