Aron Baynes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchezaji wa Mpira wa kikapu Aron Baynes
Mchezaji wa Mpira wa kikapu Aron Baynes

Aron John Baynes (alizaliwa 9 Desemba 1986) ni mchezaji wa mpira wa kikapu wa Australia ambaye mara ya mwisho alicheza kwa Raptors Toronto wa Chama cha Taifa cha Mpira wa Kikapu.

Alicheza mpira wa kikapu wa chuo kikuu cha Washington State kabla ya kuanza kazi yake ya kitaaluma huko Ulaya. Mwaka 2013, alijiunga na [1]San Antonio Spurs, na mwaka mmoja baadaye, alishinda michuano ya Chama cha Taifa cha Mpira wa kikapu na Spurs. Pia amewahi kucheza na [2]Detroit Pistons, Boston Celtics, na Phoenix Suns. Baynes pia anaichezea timu ya taifa ya Australia.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "San Antonio Spurs", Wikipedia (in English), 2021-11-19, retrieved 2021-12-02 
  2. "Detroit Pistons", Wikipedia (in English), 2021-11-29, retrieved 2021-12-02