Arkelao
Mandhari

Arkelao (23 KK - 18 BK) alikuwa mtawala wa Yudea, Idumea na Samaria kuanzia mwaka 4 KK hadi 6 BK. Alizaliwa na mfalme Herode Mkuu na Malthake akafariki Yeriko baada ya kuondolewa madarakani na Warumi kutokana na malalamiko ya Wayahudi.
Anajulikana hasa kutokana na habari inayosimuliwa katika Injili ya Mathayo (2:19-23), kwamba Yosefu alipotoka uhamishoni Misri, aliogopa kurudi Bethlehemu kwa sababu ilikuwa chini ya Arkelao, mtu mkatili mno, akaona afadhali kuhamia Nazareti, Galilaya, chini ya mdogo wake, Herode Antipa.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- ARCHELAUS by Abraham Schalit. Encyclopaedia Judaica article at Encyclopedia.com
- Herod Archelaus at Livius.org
- Archelaus by Richard Gottheil and Louis Ginzberg at The Jewish Encyclopedia
| Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Arkelao kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
