Aristarko wa Thesalonike

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aristarko wa Thesalonike

Mtakatifu Aristarko amechorwa katika mavazi ya askofu.
Feast

Aristarko (kwa Kigiriki Ἀρίσταρχος, Aristarkhos), alikuwa mkazi wa Thesalonike, Makedonia (leo nchini Ugiriki) [1], anayetajwa mara tano katika Agano Jipya hasa kama mfuasi na mwenzi wa Mtume Paulo.

Pamoja na Gaius, Mmakedonia mwingine, Aristarko alishambuliwa na umati mjini Efeso na kupelekwa kwenye kiwanja cha tamthilia [2].

Baadaye, Aristarko aliongozana na Paulo kurudi mkoa wa Asia kutoka Ugiriki [3].

Mwaka 58 aliongozana tena na Paulo kwenda Yerusalemu ili kuwakilisha mchango wa Wakristo wa kimataifa kwa wenzao maskini wa Kiyahudi.

Huko Kaisarea Baharini alipanda na Paulo meli ya kwenda Myra, Lycia [4] na kutoka huko hadi Roma.

Ndiyo sababu Aristarko anatajwa na Paulo kama "mfungwa mwenzangu"[5] na "mfanyakazi mwenzangu"[6].

Kadiri ya mapokeo alipata kuwa askofu wa Thesalonike au wa Apamea.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe tofauti: 4 Agosti[7], 4 Januari, 14 Aprili na 27 Septemba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Mdo 27:2
  2. Mdo 19:29
  3. Mdo 20:4
  4. Mdo 27:2
  5. Kol 4:10
  6. Film 1:24
  7. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aristarko wa Thesalonike kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.