Nenda kwa yaliyomo

Arik Ben Marshall

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Arik Ben Marshall (alizaliwa 13 Februari 1967)[1] ni mpiga gitaa, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mshairi na mwandishi kutoka Marekani, anayejulikana zaidi kwa kuwa mwanachama wa Red Hot Chili Peppers kati ya miaka 19921993.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Arik Ben Marshall ni wa tatu kati ya watoto watano waliozaliwa wa baba mwenye asili ya Afrika na mama Myahudi.[2]

Mwanzo wa safari ya muziki

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kutumbuiza katika maeneo mbalimbali ya Los Angeles na wanamuziki tofauti, Marshall alianza kupata kazi kama mwanamuziki wa studio, akishiriki katika kurekodi miziki ya wasanii kama Tone Loc, Etta James, na Sting.

Mwaka 1988, yeye na kaka yake Lonnie Marshall waliunda bendi waliyoita "Marshall Law". Walisaini mkataba wa maendeleo na Island Records na kurekodi demo kwa ajili yao. Bendi hiyo ilivunjika baada ya kutoa nyimbo mbili tu kwenye mkusanyiko wa Ska Parade.[3]

Baada ya kuvunjika kwa bendi, Lonnie aliunda Weapon of Choice. Marshall aliendelea kutumbuiza katika maeneo ya Los Angeles na kwa muda mfupi aliiongoza bendi yake mwenyewe iliyojulikana kama Alpha Jerk, kabla ya kuivunja na kujiunga na Red Hot Chili Peppers mwaka 1992.

Marshall Law waliungana tena mwaka 2006 na wakatoa albamu iitwayo Another X-cuse.

  1. California Births, 1905 – 1995". www.familytreelegends.com. February 13, 1967. Retrieved August 6, 2014
  2. Guitar World November 1992". Januari 5, 2013
  3. Weapon of Choice interview". www.furious.com. Retrieved August 6, 2014