Aqif Pasha Elbasani
Aqif Pasha Biçaku anajulikana zaidi kama Aqif Pashë Elbasani (1860 – 10 Februari 1926) alikuwa kiongozi wa kisiasa wa Albania wa Dola ya Kiothomani katika Sanjak ya Elbasan, na baada ya Mapinduzi ya Turki Vijana akawa mwanaharakati wa harakati za kitaifa za Albania.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Aqif Pasha alizaliwa mnamo mwaka 1860 huko Elbasan, enzi hizo ikiwa sehemu ya Vilayet ya Monastir katika Dola ya Kiothomani (leo hii Albania ya Kati, Albania). Alikuwa mtoto wa Mahmud Pertef Pasha Biçakçiu, mkuu wa moja ya familia tatu zenye ushawishi mkubwa, heshima na zilizomiliki ardhi mjini humo, na mama yake aliitwa Shefikat Hanëm Alizoti kutoka familia ya Alizoti. Dada wa mama yake alikuwa Vafsije Alizoti, mama mzazi wa Essad Pasha Toptani na Gani Toptani, jambo lililomfanya Aqif Pasha kuwa binamu wa kwanza (upande wa mama) wa Esad Pasha Toptani na Gani Toptani.[1][2] Jina la ukoo wake linatokana na neno la Kituruki bıçakçı, linalomaanisha "mtengenezaji wa visu", ikionyesha kuwa hiyo ilikuwa kazi au taaluma ya mababu zake (linaloendana na jina la ukoo wa Wabosnia la Bičakčić). Katika miaka yake ya kwanza ya shule alifundishwa faragha (nyumbani) na baadaye akapata elimu yake mjini Istanbul.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Vlora, Eqrem bej (2003). Kujtime 1885-1925. Ilitafsiriwa na Afrim Koçi. Tiranë: IDK. uk. 569. ISBN 99927-780-6-7.
- ↑ Kruja, Mustafa; Margjokaj, P. Paulin (2006). Letërkëmbim (1947-1958). Shkodër: Camaj-Pipa. uk. 373. ISBN 99943-34-47-6.
- ↑ Dervishi, Kastriot (2012). Kryeministrat dhe ministrat e shtetit shqiptar në 100 vjet. Tiranë: 55. uk. 90. ISBN 9789994356225.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Aqif Pasha Elbasani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |