Apolinari wa Hierapoli
Mandhari

Apolinari wa Hierapoli (pia: Apolinari Klaudio au Apolinari Mtetezi wa Dini; alifariki karne ya 2) alikuwa askofu aliyeongoza kanisa la Hierapoli na kumuandikia kaisari Marcus Aurelius "Apologia", kitabu cha kutetea Wakristo dhidi ya dhuluma ya Dola la Roma (177)[1].
Aliandika pia vitabu vingine dhidi ya Upagani na uzushi. Hata hivyo zimetufikia sehemu chache, ile ndefu zaidi ikihusu tarehe ya Pasaka.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Januari[2][3].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Campbell, Thomas. "St. Apollinaris Claudius." The Catholic Encyclopedia Vol. 1. New York: Robert Appleton Company, 1907. 5 September 2017
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Butler, Alban. "St. Apollinaris, the Apologist, Bishop", Lives of the Saints, vol.1, 1866
Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk 14-15
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |