Majiranukta ya kijiografia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 20:16, 8 Machi 2013 na Addbot (majadiliano | michango) (Bot: Migrating 114 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q22664 (translate me))

Anwani ya kijiografia ni namna ya kutaja mahali duniani. Anwani ya kijiografia huelezwa kwa kutaja longitudo na latitudo za mahali fulani.

Dunia hugawiwa katika gredi 360 za longitudo na gredi 180 za latitudo (90° za kaskazini na 90° za kusini).

Latitudo za kaskazini na kusini ya ikweta zinatofautishwa ama kwa kuongeza herufi "N" (=north au kaskazini) na "S" (south au kusini) au kwa alama za "+" (kaskazini) na "-" (kusini).

Gredi za longitudo zinaanza kuhesabiwa kwenye meridiani ya 0° iliyokubaliwa ni mstari kutoka ncha ya kaskazini hadi ncha ya kusini unaopita katika mji wa Greenwich (karibu na London / Uingereza).

Kwa mfano anwani ya Accra (Ghana) ni: 5°30' N (latitudo) na 0°10' W (longitudo).

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.