Antonio Barberini
Mandhari



Antonio Barberini (5 Agosti 1607 – 3 Agosti 1671) alikuwa kardinali, Askofu Mkatoliki wa Reims, kiongozi wa kijeshi, mhamasishaji wa sanaa na mshiriki maarufu wa familia ya Barberini kutoka Italia.
Kama mmoja wa kardinali-ndugu wa Papa Urban VIII na mtetezi wa Ufaransa, alichukua nafasi muhimu katika mabaraza kadhaa ya uchaguzi wa Papa katika karne ya 17.[1] Pamoja na ndugu zake Kardinali Francesco Barberini na Taddeo Barberini, alichangia katika kuunda siasa, dini, sanaa na muziki wa Italia ya karne ya 17. Wakati mwingine anajulikana kama Antonio Mdogo au Antonio Barberini iuniore ili kumtofautisha na mjomba wake Antonio Marcello Barberini.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Power And Religion in Baroque Rome: Barberini Cultural Policies by P. J. A. N. Rietbergen (Brill, 2006)
- ↑ Miranda, Salvador. "BARBERINI, seniore, O.F.M.Cap., Antonio (1569-1646)". The Cardinals of the Holy Roman Church. Florida International University. OCLC 53276621. Iliwekwa mnamo 30 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |