Antonino wa Sorrento

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu yake.

Antonino wa Sorrento (Campagna, Salerno, Italia, 555 hivi - Sorrento, Napoli, 625) alikuwa kwanza mmonaki Mbenedikto huko Monte Cassino.

Monasteri yake ilipovamiwa na Walombardi, hakukimbilia Roma kama wenzake, bali alikwenda kuishi kama mkaapweke karibu na Sorrento kwenye pwani ya Mediteranea nchini Italia.

Mwishowe akawa abati wa monasteri ya jirani[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 14 Februari[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.