Antoine Quartier
Mandhari
(Elekezwa kutoka Antoine Qaurtier)
Antoine Quartier (1632–1702) alikuwa mwandishi wa kumbukumbu kutoka Ufaransa. Alikuwa mhanga wa Biashara ya Utumwa Afrika Kaskazini (Barbary) baada ya kutekwa nyara na maharamia wa Barbary na kuuzwa nchini Libya, ambako aliishi kama mtumwa kati ya mwaka 1660 na 1668. Baada ya kurejea Ufaransa, aliandika kumbukumbu ya uzoefu wake kama mtumwa — ambayo ni miongoni mwa maelezo adimu kuhusu utumwa nchini Libya — pamoja na hadithi nyingi za watumwa walioteswa kikatili, zinazoonyesha hali ya utumwa huko Aljeria na Moroko.[1]
Alijiunga na shirika la Wamersedari huko Paris mwaka 1671, na aliwekwa wakfu kama padri baada ya Septemba 1676.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Klarer, Mario, mhr. (2022-03). Barbary Captives: An Anthology of Early Modern Slave Memoirs by Europeans in North Africa. Columbia University Press. ISBN 978-0-231-55512-8.
{{cite book}}: Check date values in:|date=(help)
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |