Nenda kwa yaliyomo

Anthony Davis

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Anthony Davis akiwa anachezea timu ya kikapu ya New Orleans Pelicans mwaka 2017
Davis akiwa na Los Angeles Lakers mnamo 2022

Anthony Marshon Davis (alizaliwa 11 Machi 1993) ni mchezaji wa mpira wa kikapu kutokea Marekani anayeichezea timu ya Los Angeles Lakers katika Chama cha mpira wa kikapu Marekani (NBA).

Davis alikuwa wa kwanza kuchaguliwa mwaka 2012 katika uteuzi wa wachezaji wa Chama cha taifa cha mpira wa kikapu(NBA). Amefanikiwa kuteuliwa katika timu ya mastaa marekani kwa mara sita. Alishinda medali ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2012 akiwa pamoja na timu yake ya Marekani.Mnamo 2021, aliteuliwa katika Timu ya Maadhimisho ya Miaka 75 ya NBA.[1] Davis anazingatiwa sana kama mmoja wa washambuliaji wakuu wa wakati wote.[2]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Anthony Davis kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "NBA 75th Anniversary Team announced". NBA.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-05-25.
  2. "20 greatest power forwards ever: The HoopsHype list". HoopsHype (kwa American English). 2022-10-02. Iliwekwa mnamo 2023-05-25.