Nenda kwa yaliyomo

Anna Kendrick

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Anna Kendrick mnamo 2016.

Anna Cooke Kendrick[1] (amezaliwa Agosti 9, 1985) ni mwigizaji wa Marekani. Anajulikana kwa kuigiza wahusika wenye mvuto na wenye bidii katika filamu za vichekesho na muziki. Tuzo na uteuzi zake zinajumuisha uteuzi wa Academy Award, Primetime Emmy Award na Tony Award.

Kendrick alipata nafasi yake ya kwanza ya uigizaji mkuu katika tamthilia ya Broadway ya mwaka 1998, High Society, ambapo aliteuliwa kwa Tony Award kama mwigizaji bora katika kipengele cha filamu ya muziki.[2] Aliigiza kwa mara ya kwanza katika filamu ya vichekesho ya muziki Camp (2003) na baadaye akapata nafasi ya msaidizi katika The Twilight Saga (2008–2011). Umaarufu wake uliongezeka zaidi kupitia filamu ya vichekesho na maigizo Up in the Air (2009), ambayo ilimletea uteuzi wa Academy Award kama Mwigizaji Bora Msaidizi, na kwa nafasi yake kama nyota katika mfululizo wa filamuza Pitch Perfect (2012–2017).

Aliigiza katika filamu za vichekesho Scott Pilgrim vs. the World (2010) na 50/50 (2011), filamu ya uhalifu End of Watch (2012), filamu ya muziki Into the Woods (2014), filamu za kusisimua The Accountant (2016) na A Simple Favor (2018), na filamu ya vichekesho ya fantasy Noelle (2019). Ameigiza sauti ya mhusika mkuu katika filamu za muziki wa katuni za Trolls tangu 2016. Pia aliigiza katika mfululizo wa vichekesho wa muda mfupi Dummy (2020), ambao ulimletea uteuzi wa Primetime Emmy Award for Outstanding Actress. Aliingia katika uongozaji wa filamu kwa mara ya kwanza kupitia filamu ya kusisimua Woman of the Hour (2023), ambayo pia aliigiza kama mhusika mkuu.

Kendrick ameimba kwenye albamu za filamu zake, ikiwa ni pamoja na wimbo "Cups" mwaka 2012, na katika matukio makubwa kama vile Kennedy Center Honors ya 2013 na Tuzo za Academy za 2015. Kitabu chake cha kumbukumbu, Scrappy Little Nobody, kilichapishwa mwaka 2016.

  1. "Anna Kendrick Biography". Biography.com. Machi 26, 2021. Iliwekwa mnamo Agosti 31, 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Anna Kendrick Says Acting Is 'The Way That I Learn About Other People'". NPR (kwa American English). Novemba 14, 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Novemba 14, 2016. Iliwekwa mnamo Novemba 1, 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]