Anna Colas Pépin
Anna Colas Pépin au Anne-Nicolas "Annacolas" Pépin (1787-1872), alikuwa mwanamke maarufu, mfanyabiashara mwenye asili ya Ulaya (baba) na Afrika (mama). Yeye ni miongoni mwa wanawake shombeshombe matajiri na maarufu katika kisiwa kidogo kiitwacho Gorée huko Senegal. Lakini mara nyingi amekua akichanganywa na shangazi yake Anne Pépin.[1]
Alikuwa binti wa Nicolas Pépin (1744–1815) na Marie-Thérèse Picard (aliyefariki 1790), aliolewa na François de Saint-Jean na akawa mama wa Mary de Saint Jean (1815–1853), mke wa Msenegali wakwanza kutumikia Bunge la Ufaransa, Barthélémy Durand, mchoro maarufu wa 184 Valantin– Édouard Auguste Nousveaux anaweza kuonyesha kuwa pichani anaweza kua Anna Colas Pépin au binti yake.[2]
Pépin alifafanuliwa kama mwanachama mkuu na mwenye ushawishi mkubwa wa jumuiya ya Signare, na aliwekeza katika ardhi na majengo huko Gorée kwa ushirikiano na mamlaka ya Ufaransa. Kama mwanachama mkuu wa wasomi wa eneo hilo, Anna kama kinara wa wasomi alimpokea kwa umaarufu François d'Orléans, mtoto wa Mfalme wa Joinville kwenye ziara yake ya Gorée mnamo 1842, tukio lililoonyeshwa na Édouard Auguste Nousveaux.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://books.google.com/books?id=O74pDwAAQBAJ&dq=Anna+Colas+P%C3%A9pin&pg=PA4
- ↑ Semley, Lorelle (2017-07-20). To be Free and French: Citizenship in France's Atlantic Empire (kwa Kiingereza). Cambridge University Press. ISBN 978-1-107-10114-2.