Nenda kwa yaliyomo

Anna Batchelor

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Anna Batchelor ni Mwingereza anayefanya kazi kama daktari mshauri (consultant physician), anayejulikana zaidi kwa mchango wake katika elimu ya tiba ya uangalizi mahututi (intensive care). Alikuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Mkuu (Dean) wa Shirika la Tiba ya Uangalizi Mahututi (Faculty of Intensive Care Medicine) kati ya mwaka 2013 hadi 2016, na pia alikuwa Rais wa Intensive Care Society kuanzia 2005 hadi 2007.[1]

Batchelor alisoma udaktari katika Chuo Kikuu cha Sheffield na akahitimu kama daktari mwaka 1980. Alipata mafunzo katika tiba ya uangalizi mahututi na anesthesiology (udaktari wa usingizi) katika Sheffield, Leicester na Newcastle, na amekuwa daktari mshauri tangu mwaka 1993. Batchelor ameongoza maendeleo ya mitaala katika tiba ya uangalizi mahututi na anesthesiology.

Batchelor ni Mwenyekiti wa sasa wa Critical Care Leadership Forum na amekuwa mwanachama wa Baraza la Royal College of Anaesthetists tangu mwaka 2008.

  1. ["Women) in medicine: Anna Batchelor and Gillian Hanson". RCP London. 2017-10-03. Iliwekwa mnamo 2018-02-22. {{cite news}}: Check |url= value (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Anna Batchelor kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.