Ann Wigmore
Ann Wigmore (4 Machi 1909 – 16 Februari 1994) alikuwa mtaalamu wa afya ya asili kutoka Lithuania na Marekani, aliyefanya kazi kama mtaalamu wa afya mbadala, mtaalamu wa tiba asili (naturopath), na mtetezi wa lishe ya vyakula vibichi (raw food).
Alikuwa ameathiriwa na nadharia za “kurudi kwenye asili” zilizoenezwa na Maximilian Bircher-Benner, na aliamini kwamba mimea huhifadhi nishati kubwa ya jua (‘Vital Force’) kuliko wanyama, na kwamba Majani machanga ya ngano inaweza kusaidia “kusafisha sumu” mwilini. Pia alipinga sana matumizi ya viambato vya kemikali katika chakula (food additives). Ingawa taasisi yake ya Ann Wigmore Foundation ilipata usajili kama shirika lisilo la faida, madai yake mengi yalipingwa na wataalamu wa afya na kuhusishwa na Ulaghai wa tiba, na elimu yake ya kitaaluma haikuthibitishwa rasmi.
Muktadha wa kihistoria
[hariri | hariri chanzo]Wigmore aliathiriwa kwa kiasi kikubwa na mawazo ya Maximilian Bircher-Benner (1867–1939), ambaye naye aliathiriwa na harakati ya Kijerumani ya Lebensreform, iliyokuwa ikikosoa ustaarabu wa kisasa na kuhimiza kurudi kwenye maisha ya asili. Harakati hiyo ilihusisha tiba asili, mazoezi, kuishi maisha ya nje, aina mbalimbali za imani za kiroho, pamoja na mitazamo ya chakula “cha asili”.[1]: 31–33
Bircher-Benner baadaye alikubali lishe ya mboga (vegetarianism), lakini alienda mbali zaidi na kuamini kuwa chakula kibichi (raw food) ndicho chakula cha asili kwa binadamu. Pia aliathiriwa na mawazo ya Charles Darwin kwamba binadamu ni aina ya mnyama kama wengine, akitazama kuwa wanyama wengine hawapiki chakula chao.[1]: 31–33
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 Fitzgerald M (2014). [Diet Cults: The Surprising Fallacy at the Core of Nutrition Fads and a Guide to Healthy Eating for the Rest of US. Pegasus Books. ISBN 978-1-60598-560-2.
{{cite book}}: Check|url=value (help)](https://archive.org/details/dietcultssurpris0000fitz}})
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ann Wigmore kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |