Nenda kwa yaliyomo

Ann-Kio Briggs

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ann-Kio Briggs inaweza pia kuandikwa kama Annkio Briggs(alizaliwa tarehe 29 Julai mwaka 1952 nchini Uingereza ) ni mwanamazingira na mwanaharakati wa haki za binadamu mwenye asili ya kinigeria aliyezaliwa Uingereza.[1][2][3] Yeye ndiye ndiye mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali liitwalo Agape Birthrights .Kufikia mwaka wa 2011, alikuwa msemaji wa Bunge la Republican la Ijaw (IRA) pamoja na United Niger Delta Energy Development Security Strategy (UNDEDSS).[4][5]

Maisha Awali na Elimu

[hariri | hariri chanzo]

Briggs alizaliwa tarehe 29 Julai mwaka 1952 nchini Uingereza. Alizaliwa na mama wa Mwingereza na mhandisi wa baharini wa Ijaw. Katika miaka yake ya awali, alipelekwa kuishi na bibi yake mzaa baba, ambaye alimlea pamoja na baba yake huko Abonnema, Jimbo la Rivers. Akiwa Abonnema, alimaliza shule yake ya msingi na kujiandikisha katika Shule ya sekondari ya Holy Rosary Girls huko mjini Port Harcourt. Kuanzia mwaka 1967 hadi 1970, masomo yake ya kitaaluma yalizuiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Baada ya vita kumalizika, Briggs alihamia Uingereza na familia yake, ambako alisoma masuala ya Masoko na kuolewa. Yeye na mume wake walijaliwa kupata watoto wanne pamoja na walitalikiana mwaka1998. Briggs anaweza kuzungumza vizuri lugha ya Igbo, na pia lugha yake ya asili, Kalabari. Pia anazungumza Kiingereza cha Pijini.[6][5]

Mnamo mwaka 1998, baada ya miaka kadhaa huko Ulaya, alirejea katika eneo la Niger Delta na kuanzisha shirika la Agape Birthright, shiririka lisilo la kiserikali,[7][6] lenye makao makuu mjini Port Harcourt, Jimbo la Rivers. Briggs, kupitia shirika lake, amesaidi baadhi ya maeneo yanayoendelea kwa kutunza kumbukumbu za usafishaji wa umwagikaji wa mafuta na kupigana dhidi ya ukosefu wa haki na kutengwa.[8] Pia anashirikiana kimataifa na mashirika mengine, ya ndani na nje ya nchi.[9][10][5]

Briggs alipokea tuzo ya Ijaw heroes kutoka kwa bunge la jamhuri ya Ijaw.[11]

  1. Our Reporter (2021-01-27). "Ann-Kio Briggs charges Ijaws to support NDDC's IMC". Tribune Online (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  2. Opejobi, Seun (2018-03-27), "Ann-Kio Briggs hails Danjuma over comment on self defence", Daily Post Nigeria (kwa American English), iliwekwa mnamo 2025-11-14
  3. "How Buhari Can End Secession Agitations — Annkio Briggs". Daily Trust (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2021-06-18. Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  4. admin (2013-09-20). "The Problem Of Niger Delta Is Few Greedy Nigerians- Ann-kio Briggs". The Newsriter (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  5. 1 2 3 Spotlight On Ann Kio Briggs, Ijaw Rights Activist (kwa American English), ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-28, iliwekwa mnamo 2025-11-14
  6. 1 2 Bolatito Adebayo. "At 59, Annkio Briggs says: Im a creek girl - nigeriafilms.com". www.nigeriafilms.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-28. Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  7. Akinlolu Oluwamuyiwa (2017-03-24). "Ann-Kio Briggs- The fight of her life". The Guardian Nigeria News - Nigeria and World News (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  8. adefaye (2013-05-19). "It's Jonathan or no peace - Annkio Briggs". Vanguard News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-11-14.
  9. Annkio Briggs (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2008-08-26, iliwekwa mnamo 2025-11-14
  10. https://web.archive.org/web/20160303214503/http://ip-50-63-126-34.ip.secureserver.net/index.php/blog/2012/06/the-other-side-of-annkio-briggs
  11. "Tompolo, Prof. Okaba, Annkio, Abbey Hart, Others Win Ijaw Heroes Awards – National Point Newspapers" (kwa American English). 2025-11-08. Iliwekwa mnamo 2025-11-14.