Angola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 08:44, 18 Septemba 2016 na DARIO SEVERI (majadiliano | michango) (Update inf. from wiki (en) + (pt) + (fr))
Angola
Ramani ya Angola
Luanda, mji mkuu wa Angola

Angola ni nchi kubwa iliyopo upande wa kusini wa bara la Afrika ikipakana na Namibia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Zambia. Upande wa magharibi kuna pwani ndefu ya Bahari Atlantiki. Mkoa wa Kabinda umetenganika na sehemu nyingine za nchi na unapakana na Jamhuri ya Kongo pia.

Angola ni nchi tajiri kwa mafuta na madini: almasi ndiyo muhimu zaidi. Lakini nchi ni maskini kutokana na vita vya miaka 29; kwanza vita vya kupigania uhuru dhidi ya Ureno iliyofuatwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe hadi mwaka 2002.

Nchi yenyewe hasa ni ya kidemokrasia na inajulikana kama Jamhuri ya Angola (kwa Kireno: República de Angola, kwa matamshi ya IPA: /ʁɛ.'pu.βli.kɐ dɨ ɐ̃.'ɣɔ.lɐ/; kwa lugha za wenyeji: Repubilika ya Ngola).

Asili na historia ya jina 'Angola'

Jina Angola linatokana na neno la lugha ya Kibantu "N’gola", ambalo lilikuwa jina la kiongozi wa ufalme wa Kwimbundo karne ya 16, ambapo Wareno walianza ukoloni katika eneo hili.

Jiografia

Maeneo ya Angola

Ramani ya Angola na Mikoa iliohesabiwa
Ramani ya Angola na Mikoa iliohesabiwa
Makala kuu: Mikoa ya Angola
,
Makala kuu: Manispaa za Angola

Angola imegawiwa katika mikoa 18 (províncias) na manispaa 162 (municípios).
Mikoa ni:

Historia

Makala kuu: Historia ya Angola

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK kutoka kaskazini walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Kuanzia karne ya 14, falme mbalimbali zilienea sehemu za Angola, kwa mfano Dola la Kongo, Dola la Lunda na Dola la Kasanje.

Dola la Kongo

Ramani ya kihistoria ya Kongo

Dola la Kongo lilikuwa ufalme ulioenea ndani ya nchi za leo za Angola, Kongo (Kinshasa) na Kongo (Brazzaville).

Ulianzishwa katika karne ya 14 ikadumu hadi karne ya 17.

Mtawala wake alikuwa na cheo cha "Mwene Kongo" au "Manikongo" wa kabila la Bakongo.

Ufalme huo umejulikana zaidi kihistoria kwa sababu ya mawasiliano yake ya kimataifa. Katika karne ya 15 meli za Wareno zilifika mwambaoni mwake.

Wakati wa kukutana na Wareno Ufalme wa Kongo labda ulikuwa na eneo la km² 300,000 ukaunganisha robo ya magharibi ya Kongo (Kinshasa) pamoja na sehemu za Angola na Kongo (Brazzaville).

Manikongo mbalimbali walijenga uhusiano na Ureno na Kongo ilikuwa taifa la kushikamana na Ureno hadi kuharibika kwa uhusiano huo. Katika kipindi kile taarifa mbalimbali ziliandikwa zinazotupa leo picha nzuri ya ufalme huo.

Manikongo alikaa katika mji wa M'banza-Kongo.

Baada ya wafalme kuwa Wakristo Wakatoliki na kujengwa kwa kanisa kuu, jina la "São Salvador do Congo" (kwa Kireno: "Mwokozi Mtakatifu wa Kongo") lilikuwa kawaida kwa mji mkuu wa milki.

Ufalme ukawa na majimbo, wilaya na vijiji. Majimbo yalikuwa saba ya Mpemba, Nsundi, Mpangu, Mbata, Mbamba na Soyo.

Kwa mikataba ya baadaye falme za Kakongo, Loango na Ngoy likatokea shirikisho ya sehemu nne.

Dola la Lunda

Dola la Lunda lilikuwa ufalme wa Kibantu katika miaka 1600 hadi 1850 hivi kandoni kwa mto Kasai, mpakani kwa nchi za kisasa za Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Dola la Kasanje

Dola la Kasanje lilikuwa ufalme wa Kibantu katika miaka 1620 hadi 1910 hivi kandoni kwa mto Kwango, upande wa kaskazini wa nchi ya kisasa ya Angola. Lilianzishwa na viongozi kutoka Dola la Lunda.

Mwaka 1910 lilivamiwa na Wareno na kuingizwa katika koloni lao la Angola.

Siasa

Kaulimbiu ya Angola ni "Virtus, Unita Fortior", kumaanisha "umoja utupe nguvu"

Watu

Wakazi wengi ni Waafrika, hasa wa makabila ya Waovimbundu (37%), Waambundu (25%) na Wakongo (13%). Machotara ni 2%, Wachina 1,4% na Wazungu 1%.

Ingawa lugha za Kibantu zinaongoza, na 6 kati yake zina hadhi ya lugha ya taifa, lugha rasmi ni Kireno.

Upande wa dini, inakadiriwa kuwa zaidi ya nusu ni Wakatoliki na robo ni Waprotestanti wa madhehebu mia tofauti.

Angalia pia

Tanbihi

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Serikali

Habari

  • allAfrica - Angola - viungo via habari
  • Angola Press -idara ya Taarifa na habari ya Angola (kwa kireno, kifaransa na kingereza)
  • Angonoticias (kwa kireno) -lango la habari lenye sifa Angola
  • Mangole (kwa kireno) - ya habari nchini Angola na pia maelekezo ya makala kwa kompyuta.
  • Jornal de Angola (kwa kireno) - Gazeti lenye sifa Angola

Maoni

Radio na Muziki

Maelekezo

Utalii

Mambo mengine


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Angola kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.