Nenda kwa yaliyomo

Angelique Gerber

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Angelique Gerber (alizaliwa 16 Aprili 1983) ni mwigizaji wa Afrika Kusini ambaye alizaliwa, anaishi na kufanya kazi Johannesburg. Aliwahi kukaa kwa muda nchini Kanada kuanzia mwaka 2001 hadi 2002 kwa ajili ya kurekodi filamu ya Disposable Life.[1] Alisoma katika shule ya sekondari ya Hoërskool Hugenote huko Springs na anajulikana zaidi kwa nafasi yake katika tamthilia ya 7de Laan kama Clara.[2] Katika tamthilia ya 7de Laan anaigiza kama Clara, msichana kijana kutoka Bucharest, Romania ambaye huzungumza Kiafrikana kwa kusitasita na wakati mwingine hupata ugumu wa kujieleza ipasavyo. Pia alikuwa na nafasi muhimu katika filamu ya Kanada ya mwaka 2002 Disposable Life akiigiza kama Emily.

Aidha, aliwahi kuwa mtangazaji wa tamthilia ya Boer soek 'n vrou kwenye chaneli ya KykNet.

  1. https://www.imdb.com/title/tt0240453/
  2. https://www.angeliquegerber.co.za/