Angeline Ndayishimiye
| Angeline Ndayishimiye | |
|---|---|
| | |
| Alizaliwa | 1976 |
| Nchi | Burundi |
| Kazi yake | Mke wa Raisi |
| Ndoa | Évariste Ndayishimiye |
| Watoto | 6 |
Angeline Ndayishimiye Ndayubaha (alizaliwa 1976) [1] alikua Mke wa Raisi wa Burundi mwaka 2020. Mwaka 2023 alipewa Tuzo na Umoja wa Mataifa ya Idadi ya Watu.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Alikuwa luteni alipoondoka katika jeshi mwaka 2004. [2] Mwaka 2005, alianza kufanya kazi katika Société Burundaise de Gestion des Entrepôts et d'Assistance des Avions en Escale (SOBUGAE), kampuni ya Burundi inayojiusisha na usafirishaji wa mizigo kwa ndege. Kuanzia 2010 hadi 2012, aliongoza idara ya rasilimali watu na utawala wa kampuni hiyo, na baadaye akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Utawala na Fedha. Alipata mapumziko ya mwaka mmoja katika Air Burundi lakini vinginevyo alishikilia wadhifa huu hadi 2018.
Mnamo 2017, alianzisha shirika linaloitwa Femmes Intwari ambalo lengo lake ni kukuza amani ya kidemokrasia. Wanachama wa Femmes Intwari ni wanawake ambao, kama yeye, wamewahi kutumikia jeshi au ni wajane wa wanajeshi wa Burundi. Mwaka 2019, alianzisha na kuwa raisi wa shirika la Umugiraneza ambalo linafanya kazi za kupunguza umaskini kwa kuzingatia watoto na wajane. Umugiraneza hutoa huduma za afya, kazi za kulipwa, elimu na mafunzo.
Mnamo 18 Juni 2020, alikua Mke wa Raisi wa Burundi.[3].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "H.E Madam Angeline Ndayubaha – AFLPM" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-01-16. Iliwekwa mnamo 2024-06-21.
- ↑ z.janati (2022-11-27). "sommet UA: Mme Angeline NDAYISHIMIYE, Première Dame du Burundi, âme de battante". NWL - FAAPA (kwa Kifaransa). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-03-02. Iliwekwa mnamo 2024-03-02.
- ↑ "H.E Madam Angeline Ndayubaha – AFLPM" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-05-12. Iliwekwa mnamo 2024-03-02.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Angeline Ndayishimiye kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |