Nenda kwa yaliyomo

Angelina Baiden-Amissah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Angelina Baiden-Amissah
Amezaliwa8 Februari 1954
UtaifaMgana
Kazi yakeMwanasiasa
Anajulikana kwa ajili yaUbunge na Naibu waziri wa Elimu, Vijana na michezo kati ya mwaka 2001 na 2005

Angelina Baiden-Amissah alizaliwa 8 Februari 1954 nchini Ghana, ni mwanasiasa wa Ghana na aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Shama katika Mkoa wa Magharibi wa Ghana[1]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Baiden-Amissah alizaliwa Shama, Ghana katika Mkoa wa Magharibi, na alisoma katika Shule ya Sekondari ya Mfantsiman Girls’ Senior High School.[2]

Mnamo mwaka 1991, alipata Shahada ya Elimu (Bachelor of Education) katika Somo la Sayansi ya Nyumbani (Home Economics) na Sayansi Jumuishi kutoka Chuo Kikuu cha Elimu. Baadaye alipata Cheti cha Uzamili (Postgraduate Certificate) wa “uongozi katika Maendeleo: Kusimamia Mabadiliko ya Kisiasa na Kiuchumi” kutoka Chuo Kikuu cha Harvard.

Pia alipata Shahada ya Uzamili ya Utendaji katika Usimamizi wa Biashara (Executive Master of Business Administration – EMBA) kutoka Taasisi ya Ghana ya Usimamizi na Utawala wa Umma (Ghana Institute of Management and Public Administration), pamoja na vyeti vingine katika taaluma ya Ufundishaji (Pedagojia) na Maendeleo ya Awali ya Mtoto.[3]

Baiden-Amissah alichaguliwa mwaka 2000 kuwa Mbunge wa Jimbo la Shama ndani ya Bunge la Jamhuri ya nne ya Ghana. 2004 alishinda tena uchaguzi kuipitia chama Cha NPP (New Patriotic Party) lakin alipoteza kiti chake mwaka 2008, pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Vijana na Michezo kati ya mwaka 2001 na 2005.[4][5][6]

  1. "Baiden-Amissah, Angelina". Ghana MPS (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
  2. "Baiden-Amissah, Angelina". Ghana MPS (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
  3. "Ghana Embassy to The Holy See - Bio Ambassador". www.ghanaembassyholysee.it. Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
  4. "Ghana Election shama Constituency Results". www.graphic.com.gh. Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
  5. "Baiden-Amissah, Angelina". Ghana MPS (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
  6. "Baiden-Amissah, Angelina". Ghana MPS (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.