Angastrato

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tabakastrato katika angahewa

Angastrato (pia tabakastrato, kwa Kiingereza: stratosphere) ni tabaka mojawapo la angahewa ya Dunia[1]. Inaanza takriban kilomita 8 juu ya uso wa ardhi kwenye eneo la ncha za Dunia lakini juu ya ikweta inaanza kwa kimo cha kilomita 18; inaendelea hadi kimo cha kilomita 50 juu ya uso wa ardhi[2].

Katika angastrato, kiunyume na angatropo, halijoto inapanda juu pamoja na kimo. Hii inasababishwa na tabaka la ozoni iliyoko ndani yake. Ozoni hufyonza mnururisho wa urujuanimno kutoka nuru ya Jua na kuibadilisha kuwa joto[3].

Hii ni tofauti na angatropo iliyoko chini yake. Huko halijoto inapungua kadiri ya kuongezeka kwa kimo. Pia katika angameso iliyoko juu ya tabakastrato halijoto inapungua kadiri ya kufikia juu zaidi.

Hakuna upepo wala mawingu katika angastrato, hivyo eropleni kubwa husafiri pale inapoanza kwenye kimo cha km 12 kwa safari za mbali ambako vurugu kutokana na upepo wa angatropo zimeshapungua [4].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [https://www.merriam-webster.com/dictionary/stratosphere Stratosphere], Merriam Webster dictionary
  2. The Stratosphere - overview (en). University Corporation for Atmospheric Research.
  3. The Stratosphere - overview (en). University Corporation for Atmospheric Research.
  4. Altitude of a Commercial Jet. Hypertextbook.com.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Angastrato kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.