Anfilogino Guarisi
| Anfilogino Guarisi | |
| Amezaliwa | 6 Desemba 1905 São Paulo, Brazil |
|---|---|
| Amekufa | 8 Juni 1974 (umri 68) São Paulo, Brazil |
| Nchi | Brazil |
Amphiloquio Guarisi Marques (26 Desemba 1905 – 8 Juni 1974) alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu wa Italia na Brazil aliyecheza nafasi ya mshambuliaji. Nchini Brazil alijulikana kama Filo na nchini Italia alijulikana kama Anfilogino Guarisi. Katika kazi yake, alicheza soka katika nchi zote mbili za Brazil na Italia, akiziwakilisha timu zote mbili katika ngazi ya kimataifa, na alikuwa mchezaji wa timu ya Italia iliyotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la FIFA mnamo mwaka 1934.
Kazi ya soka
[hariri | hariri chanzo]Guarisi alizaliwa mjini Sao Paulo, na mnamo mwaka 1922 alianzia kazi yake ya soka katika klabu ya Portuguesa, ambapo baba yake, Manuel Augusto Marques, alikuwa rais wa klabu hiyo.
Mnamo mwaka 1925, alihamia klabu ya Paulistano, ambapo alicheza pamoja na mchezaji maarufu Arthur Friedenreich. Katika mwaka huo huo, kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Ufaransa barani Ulaya, alifunga miongoni mwa mabao wakati Paulistano ilipoifunga Ufaransa mabao 7 kwa 2 ilikuwa kwenye ziara barani ulaya.
Mnamo 6 Desemba 1925, alicheza mechi yake ya kwanza katika timu ya taifa ya Brazil dhidi ya Paraguay. Brazil ilishinda mabao 5–2, na Filo alifunga bao mojawapo. Alikuwa mchezaji wa timu ya Brazil iliyoshika nafasi ya pili katika mashindano ya Amerika Kusini mwaka 1925.
Akiwa na Paulistano, alishinda ubingwa wa ligi ya soka ya jimbo la Sao Paulo mwaka 1926 (ambapo alikuwa mfungaji bora akiwa na mabao 16), 1927, na 1929 katika Ligi ya Soka ya ridhaa. Mnamo mwaka 1929, pia alikuwa bingwa akiwa na Corinthians kupitia chama cha michezo cha Athletico Paulista (katika miaka hiyo, kulikuwa na ligi mbili za soka huko Sao Paulo). Mnamo mwaka 1930, alishinda ubingwa mwingine wa ligi ya soka ya jimbo la Sao Paulo akiwa na Corinthians.
Alitarajia kwenda kwenye Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 1930 nchini Uruguay, lakini mzozo mkubwa kati ya ligi za soka za Rio de Janeiro na Sao Paulo ulisababisha wachezaji kutoka Rio pekee kwenda kwenye mashindano hayo. Filo, Friedenreich, na wachezaji wengine kutoka Sao Paulo hawakwenda Uruguay. Mchezaji pekee kutoka Sao Paulo aliyepata nafasi ya kwenda kwenye Kombe la Dunia alikuwa Araken, ambaye alikuwa na mgogoro na klabu yake ya Santos.
Mnamo mwaka 1931, Filo alihamia Lazio. Nchini Italia, alijulikana kwa jina lake la mwisho, Guarisi. Katika klabu hiyo, alicheza pamoja na wachezaji wengine wenye asili ya Italia na Brazil kutoka familia ya Fantoni: Ninao (Fantoni I), Nininho (Fantoni II), na Niginho (Fantoni III). Kikosi hicho cha Lazio kilijulikana kama "Brasilazio".
Mnamo mwaka 1932, Guarisi, akiwa mtoto wa mama Muitali, alipata uraia wa Italia na alichaguliwa kwenye timu iliyoshika nafasi ya pili katika kombe la kimataifa la ulaya Kati la 1931–32 na baadaye timu iliyotwaa ubingwa wa kombe la kimataifa la ulaya Kati la 1933–35, pamoja na kikosi cha Kombe la Dunia la FIFA cha mwaka 1934, na hivyo kuwa mchezaji wa kwanza kuzaliwa nchini Brazil kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia. Katika mechi pekee ya mchujo ya Kombe la Dunia iliyochezwa na Italia (dhidi ya Ugiriki), Guarisi alifunga bao la kwanza la Italia katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.[1] Katika mechi hiyo, alicheza pamoja na mchezaji mwenzake wa Lazio, Fantoni II.[1]
Alirejea Corinthians na kushinda ligi ya soka ya jimbo la Sao Paulo ya mwaka 1937. Taji lake la mwisho la Paulista lilikuwa na klabu pinzani ya Palestra Italia (ambayo sasa ni Palmeiras), timu ya soka ya jamii ya Waitalia mjini Sao Paulo.