Nenda kwa yaliyomo

Andrew Grove

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Andrew Grove

Grove mwaka 2009
Amezaliwa (1936-09-02)Septemba 2, 1936
Budapest, Hungaria
Elimu Chuo cha Jiji la New York (Shahada ya Sayansi)
Chuo Kikuu cha California, Berkeley (PhD)
Watoto 2[1]
Tuzo Tuzo ya J. J. Ebers (1974)
Time Mtu wa Mwaka, 1997
Jarida la Chief Executive, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwaka, 1997

Andrew "Andy" Stephen Grove (2 Septemba 1936 – 21 Machi 2016) alikuwa mfanyabiashara na mhandisi Mmarekani mwenye asili ya nchi ya Hungaria ambaye alihudumu kama Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa tatu wa Intel Corporation. Aliondoka Hungaria wakati wa mapinduzi ya mwaka 1956 akiwa na umri wa miaka 20 pekee na kuhamia nchini Marekani, ambako alimalizia masomo yake. Alikuwa mfanyakazi wa tatu kuajiriwa na hatimaye Afisa Mtendaji Mkuu wa tatu wa "ntel", akibadilisha kampuni hiyo kuwa kampuni kubwa zaidi duniani.[2]

Kutokana na kazi yake ndani ya Intel, pamoja na vitabu na makala zake za kitaalamu, Grove alikuwa na ushawishi mkubwa katika viwanda vya utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki duniani kote.[3] Mnamo mwaka 1997, jarida la Time lilimchagua kama mtu hodari, kwa kuwa mtu aliyechangia zaidi ukuaji wa kustaajabisha wa nguvu na uwezo wa ubunifu wa chipu za kompyuta .[4][5] Chanzo kimoja kinabainisha kuwa kwa mafanikio yake ndani ya Intel pekee, anastahili nafasi sawa na viongozi wakuu wa biashara wa karne ya 20.[6]

  1. ↑ "Former Intel chief Andrew Grove dies aged 79" BBC, Machi 22, 2016.
  2. ↑ "Andrew Grove". Bloomberg.com. 2016. Iliwekwa mnamo Juni 14, 2026.
  3. ↑ Gaither, Chris (Novemba 12, 2001). "Intel's Former Chief Speaks Out on Innovation". The New York Times. Iliwekwa mnamo Juni 14, 2026.
  4. ↑ "Andrew S. Grove, Intel Chief, Dies at 79". The New York Times. Machi 21, 2016. Iliwekwa mnamo Juni 14, 2026.
  5. ↑ "Man of the Year: Andrew Grove". Time. Desemba 29, 1997. Iliwekwa mnamo Juni 14, 2026.
  6. ↑ Movers and Shakers: the 100 Most Influential Figures in Modern Business. Basic Books. 2003. ku. 205–207.
Makala hii kuhusu wakimbizi au masuala ya ukimbizi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Andrew Grove kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.