Nenda kwa yaliyomo

Andreas Amrhein

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Padri Andreas Amrhein.

Andreas Amrhein, OSB (1844 - 29 Desemba 1927) alikuwa mmonaki padri wa Uswisi aliyeanzisha Shirika la Kibenedikto la Mt. Otilia[1] na lile la Masista Wabenedikto Wamisionari wa Tutzing ili kuunganisha maisha ya kitawa kadiri ya kanuni ya Mt. Benedikto na umisionari[2]. Mashirika hayo yalitekeleza mpango huo hasa Dar es Salaam na kusini mwa Tanzania ya leo.

Kuhusu jambo hilo, tarehe 18 Aprili 1887 Amrhein alimuandikia hivi Papa Leo XIII kuhusu mazungumzo yake na Karl Peters: "Wao wanataka wamisionari kwa ajili ya faida yao wenyewe. Lakini nimeweka masharti: wamisionari wafanye kazi yao kwa uhuru wote, bila kupingwa kwa namna yoyote na wakoloni. Licha ya hayo naona kwamba wamisionari wataweza kuwalinda wenyeji wasinyonywe ovyo na wakoloni na wafanyabiashara" [3].

  1. ""History", Benediktinerkongregation von St. Ottilien". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-02-09. Iliwekwa mnamo 2026-06-11.
  2. Dysinger, O.S.B., Luke. "Andreas Amrhein", The Benedictine Missionary Movement, St. Andrew's Abbey, Valyermo, 1990
  3. Kanisa katika Tanzania, V2, Kitabu cha Mwalimu, Ndanda Mission Press, 1975, uk. 22.