André Brink

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

André Philippus Brink (Vrede, 29 Mei 19356 Februari 2015) alikuwa mwandishi wa riwaya kutoka Afrika Kusini. Aliandika kwa lugha ya Kiafrikana na Kiingereza na alikuwa Profesa wa Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Cape Town.

Katika miaka ya 1960, yeye na Breyten Breytenbach walikuwa watu muhimu katika harakati ya uandishi wa Kiafrikana iliyoitwa Die Sestigers ("Wa miaka ya sitini"). Waandishi hao walitazamia kutumia Kiafrikana kama lugha ya kuongea dhidi ya serikali ya ubaguzi wa rangi, na pia kufanya fasihi ya Kiafrikana kusukumwa na mienendo ya wakati huo ya fasihi ya Kiingereza na Kifaransa.

Riwaya yake Kennis van die aand ("Maarifa ya Usiku ") (1973) ilikuwa riwaya ya kwanza kupigwa marufuku na serikali ya Afrika Kusini.

Brink aliandika vitabu vyake kwa wakati mmoja katika lugha za Kiingereza na Kiafrikana.

Riwaya za mapema za André Brink mara nyingi zilijihusisha na sera za ubaguzi wa rangi. Maandiko yake ya mwisho yanahusu masuala mapya ya kimaisha katika kipindi baada ya ubaguzi nchini Afrika Kusini.

Mwanawe, Anton Brink, ni mchoraji.[1]

Vitabu[hariri | hariri chanzo]

Kwa orodha kubwa zaidi ya machapisho, angalia makala haya ya Kiafrikana André P Brink.

Riwaya[hariri | hariri chanzo]

André Brink.
 • Balozi
 • Kutazama Giza
 • Wakati katika Upepo
 • Fununu za Mvua
 • Msimu Mkavu na Mweupe
 • Nyororo ya Sauti
 • Ukuta wa Ugonjwa Mkubwa
 • Hali ya Kidharura
 • Teno la Hofu
 • Maisha ya Kwana ya Adamastor (1993)
 • Kinyume na Hayo
 • Kuota kuhusu Mchanga
 • Bonde la Shetani
 • Haki za Kutamani
 • Anderkant die Stilte (2002), ilitafsiriwa kama Upande Mwingine wa Kimya
 • Kabla Nisahau (2004)
 • Upande Mwingine wa Kimya (2004)
 • Panzi (2005)
 • Mlango wa Buluu (2006)
 • Maisha Mengine (2008)

Vitabu Kuhusu Maisha[hariri | hariri chanzo]

 • Barabara yenye njia mbili (2009)
  • Iliripotiwa katika Hope, Christopher (31 Januari 2009). "Traitor to the Tribe". The Guardian. Iliwekwa mnamo 2 Juni 2009.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. "anton brink". South Africian Artists. Iliwekwa mnamo 2008-06-27.
 • Chapman, Michael. 2003. Southern African Literatures, University of Natal Press. ISBN 1-86914-028-1

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]