Anastasia Goryacheva
Anastasia Goryacheva ni mcheza ballet maarufu kutoka Urusi na soloist wa Ballet ya Bolshoi.[1]
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Goryacheva alizaliwa mjini Moscow, Russia. Mnamo mwaka 1998, alihitimu kutoka Chuo cha Choreography cha Moscow na mwaka huo huo akawa mshiriki wa Bolshoi Theatre. Mnamo mwaka 1999, alicheza katika maonyesho mengi ya Vladimir Vasiliev ikiwemo Giselle na Swan Lake ambapo alichukua nafasi ya Maid of Honour. Kutoka mwaka 2000 hadi 2003, alicheza katika maonyesho mengi ya Yuri Grigorovich, akiwemo nafasi ya Neapolitan Bride katika Swan Lake na Giselle katika baleti ya jina lile lile. Mnamo mwaka 2009, alicheza nafasi ya Swanilda katika Coppélia na mwaka mmoja kabla ya hapo alishiriki katika maonyesho ya Alexei Ratmansky kama vile Flames of Paris ambapo alicheza nafasi ya Adeline na Zina katika the Limpid Stream.[2]
Mnamo mwaka 2024, Goryacheva alistaafu kutoka kwenye jukwaa la kucheza. Kuanzia mwaka 2023, amekuwa mwalimu wa baleti katika Bolshoi Ballet.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Anastasia Goryacheva". Bolshoi Ballet. Iliwekwa mnamo 27 Juni 2019.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Anastasia Goryacheva". Bolshoi Ballet. Iliwekwa mnamo 27 Juni 2019.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Anastasiya Goryacheva". Bolshoi Theatre. Iliwekwa mnamo 19 Aprili 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Anastasia Goryacheva kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |