Nenda kwa yaliyomo

Ana Colovic Lesoska

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ana Čolović Lešoska (aliyezaliwa 1979) ni mwanabiolojia wa Jamhuri ya Masedonia Kaskazini ambaye tangu mwaka 2011 amekuwa akifanya kampeni dhidi ya ujenzi wa mabwawa kwa ajili ya uzalishaji wa umeme wa maji katika mbuga ya kitaifa ya Mavrovo ili kulinda aina za mimea na wanyama zilizo hatarini, ikiwemo Balkan lynx.[1]Hii ilipelekea na kusababisha kuondolewa kwa mikopo kutoka benki kuu ya dunia na benki ya ulaya katika ujenzi na maendeleo (EBRD), na kushawishi serikali ya Kaskazini Masedonia  kusimamisha kazi zaidi ya mabwawa katika mbuga ya kitaifa. Kwa kutambua juhudi zake, mwezi Aprili 2019 alikuwa mmoja wa wanamazingira sita waliotunukiwa Tuzo ya Mazingira ya Goldman.[2]

Colovic Lesoska, mwanabiolojia, alisikia kuhusu mipango ya kuunda mitambo ya kuzalisha umeme kwa maji huko Mavrovo mwaka wa 2010. Ilijumuisha bwawa la Boškov lenye urefu wa mita 33 na bwawa la Lukovo lenye urefu wa mita 70. Kama mkurugenzi mtendaji wa Eko-svest, kituo cha utafiti wa mazingira cha Makedonia, kwa ushirikiano na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali na wanaharakati, alizindua kampeni ya "Save Mavrovo".Mnamo Novemba 2011, aliwasilisha malalamiko kwa ERBD, akieleza kwamba walikuwa wameidhinisha mkopo wa mradi wa Boškov bila kufanya tathmini inayohitajika ya bayoanuwai. Aliwahimiza mabalozi wa nchi zilizo na wawakilishi kwenye bodi ya EBRD kushinikiza kukomeshwa ufadhili huo. Ombi alilozindua akiitaka serikali, ERBD na Benki ya Dunia kuhitimisha miradi hiyo liliungwa mkono kwa sahihi karibu 100,000.

Mnamo mwaka wa 2013, aliwasilisha malalamiko kwenye mkataba wa Berne juu ya uhifadhi wa wanyamapori na makazi asili ya ulaya, akielezea kuwa mradi wa umeme wa maji wa Boškov "unaweza kuwa na matokeo hasi kwa lynx". Mnamo desemba 2015, mkataba wa Berne uliamuru ERBD na Benki ya Dunia kusimamisha ufadhili kwani mradi unaweza kuwa na "athari hasi kwa lynx".Benki ya Dunia mara moja iliondoa ufadhili na mnamo mwezi Mei uliofuata uamuzi wa mahakama wa kubatilisha kibali cha mazingira cha mradi wa Boškov ulitolewa. Mnamo Januari 2017, EBRD ilighairi ufadhili.

Kwa kutambua mafanikio haya, mnamo Aprili 2019 Ana Colovic Lesoska alitunukiwa tuzo ya mazingira ya Goldman. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Macedonia ya Kaskazini kupewa tuzo hiyo.

  1. https://www.ebrd.com/downloads/integrity/Boskov_Most_final.pdf
  2. This year is the 30th anniversary of the prestigious Goldman Environmental Prize, the annual award honors grassroots environmental heroes from six continental regions: Europe Also called the Green Nobel Prize, Bayarjargal Agvaantseren from Mongolia This year’s winners are Alfred Brownell from Liberia (2019-04-29). "Meet the winners of the 2019 Goldman Environmental Prize". Mongabay Environmental News (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-10-04.{{cite web}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)