Amir Nour
| Amir Nour | |
| Amezaliwa | 26 Aprili, 1936 Shendi, Sudan |
|---|---|
| Amekufa | 2021 Chicago, America |
| Asili yake | Sudan |
| Kazi yake | Mchongaji (Sculpture) na Mwalimu |
| Elimu | Chuo Kikuu cha London, Chuo Kikuu cha Yale na Chuo Kikuu cha St. Andrews |
Amir Nour (Aprili 1936 – 2021) alikuwa mchongaji na msomi wa sanaa wa asili ya Sudan na Marekani. Kazi zake zimeonyeshwa nchini Marekani na kimataifa, ikiwemo Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Cuba na Falme za Kiarabu.[1]
Baada ya kupata shahada kutoka Chuo Kikuu cha London, Chuo Kikuu cha Yale na Chuo Kikuu cha St. Andrews, alifanya kazi ya kufundisha sanaa ya Fine Art huko Chicago, ambako aliishi hadi mwisho wa maisha yake mwaka 2021.[2]
Wasifu na taaluma ya kisanii
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1957, Nour alihitimu kutoka Shule ya Sanaa ya Fine and Applied Art huko Khartoum, na baadaye akawa mwalimu wa sanaa kuanzia 1958 hadi 1959 na pia kuanzia 1963 hadi 1965. Baada ya hapo, alisomea uchongaji (sculpture) na sanaa ya Afrika katika Slade School of Fine Art ya Chuo Kikuu cha London, Uingereza, na pia katika Royal College of Art jijini London.[3]
Mwaka 1967, alipata ufadhili wa masomo wa Rockefeller ili kuendelea na masomo ya uchongaji na lithografia katika Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani, ambapo alihitimu na kupata Shahada ya Kwanza na Shahada ya Uzamili katika Sanaa (Fine Arts). Baada ya hapo, alifanya kazi kama mwalimu wa sanaa katika City Colleges of Chicago.[4]
Mwaka 2006, alichukua likizo ya masomo (sabbatical leave) na kupata Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Historia ya Sanaa ya Afrika kutoka Chuo Kikuu cha St. Andrews nchini Scotland[5]
Maisha yake
[hariri | hariri chanzo]Nour alikuwa amemuoa Ann Morrison kutoka Edinburgh, Scotland ambaye alikutana nae alipokuwa mwanafunzi London. Ann alikuwa Mtaalamu wa tiba ya viungo (physical therapist) katika Taasisi ya Urekebishaji ya Schwab, na kuanzia mwaka 1980 alikuwa Mkurugenzi wa Tiba ya Urekebishaji (Rehab Medicine) katika Hospitali ya Osteopathic iliyoko Hyde Park, Chicago.[6]
Amir Nour alifariki dunia mjini Chicago mwaka 2021, akiwa na umri wa miaka 84.[7]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://africa.si.edu/exhibits/dialogue/nour.htm
- ↑ https://africa.si.edu/exhibits/dialogue/nour.htm
- ↑ https://www.hpherald.com/obituaries/amir-nour-patient-sculptor-of-contemporary-african-art-dies-at-84/article_830fccd0-c7b1-11eb-9459-d7d59a03a13e.html
- ↑ https://www.amirnour.com/about
- ↑ https://www.hpherald.com/obituaries/amir-nour-patient-sculptor-of-contemporary-african-art-dies-at-84/article_830fccd0-c7b1-11eb-9459-d7d59a03a13e.html
- ↑ https://africa.si.edu/exhibits/dialogue/nourI.htm
- ↑ https://www.hpherald.com/obituaries/amir-nour-patient-sculptor-of-contemporary-african-art-dies-at-84/article_830fccd0-c7b1-11eb-9459-d7d59a03a13e.html
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Amir Nour kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |