Nenda kwa yaliyomo

Amina Chifupa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hayati Amina Chifupa

.

Amina Chifupa Mpakanjia (20 Mei 1981 - 26 Juni 2007) alikuwa Mbunge wa kiti maalum kupitia tiketi ya Vijana na alikuwa kiongozi anayepiga vita dhidi ya utumiaji na uuzaji wa madawa ya kulevya.

Alisoma shule ya msingi Ushindi na kujiunga na masomo ya sekondari Kisutu kabla ya kuingia shule nyingine ya sekondari ya Makongo alikomaliza elimu ya kidato cha sita mwaka wa 2002.

Kabla ya kumaliza masomo yake Amina alikuwa mtangazaji wa redio iitwayo Clouds FM, katika kipindi akiwa mtangazaji aliweza kuvuma sana kutokana na sauti yake iliyokua nyororo na ya kuvutia haswa kwa vijana wenzake. Aliendelea na kazi hii ya utangazaji pale alipomaliza masomo yake hadi alipoteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu katika serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania awamu ya nne.

Mumewe alikuwa akiitwa Mohammed Mpakanjia ambaye pia ameshatangulia mbele za haki.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amina Chifupa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.