Amina Benbouchta
| Amina Benbouchta | |
|---|---|
| Amezaliwa | 1963 |
| Kazi yake | msanii |
Amina Benbouchta (alizaliwa 1963) ni msanii kutoka Moroko anayejihusisha na uchoraji wa picha, upigaji picha na sanaa ya maonesho ya vitu. Alisoma nchini Kanada na Paris, na anatambulika kimataifa kwa kazi zake za sanaa za kisasa zinazojikita katika masuala ya kijamii, hasa yale yanayohusiana na siasa za jinsia.Katika hatua za awali za kazi yake, aliwahi kuongoza jarida la mitindo na utamaduni liitwalo Les Aligés. Pia alikuwa miongoni mwa wanachama wa kikundi cha wasanii na wakurugenzi wa sanaa cha Collectif 212, ambacho kilijikita katika kusaidia na kukuza sanaa ya kisasa ya wasanii chipukizi nchini Morocco.[1]
Elimu na kazi
[hariri | hariri chanzo]Amina Benbouchta alizaliwa mwaka 1963 mjini Casablanca, Morocco, na alikulia katika kipindi kilichojulikana kama “Miaka ya Mateso”[2] chini ya utawala wa Mfalme Hassan wa Pili wa Morocco ,kipindi kilichotambulika kwa vurugu za dola na ukandamizaji wa kisiasa.Katika kipindi hicho ndipo alianza rasmi kazi yake ya sanaa mwaka 1986, baada ya kumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha McGill huko Montreal, Canada, ambako alisomea Anthropolojia na masomo ya Mashariki ya Kati.Baadae, mwaka 1988, aliendelea kujifunza sanaa kwa kuhudhuria masomo kama msikilizaji hapo École Nationale des Beaux-Arts huko Paris kwa muda wa miaka miwili.Kazi zake za sanaa zimeoneshwa katika taasisi mbalimbali duniani, kuanzia Maonesho ya Cairo Biennial (1993) hadi Makumbusho ya Kitaifa ya Wanawake na Sanaa huko Washington DC, Marekani (1997). Maonesho yake ya hivi karibuni ya pamoja na ya binafsi yamefanyika Rabat, Morocco. Kwa ujumla, amekuwa akiwasilisha kazi zake zaidi huko Morocco, Hispania na Ufaransa, na alianza kushiriki maonyesho ya biashara ya sanaa mwaka 2008 huko Marakesh[3].
Katika miaka ya 1990, Benbouchta aliwahi kuongoza jarida la mitindo na utamaduni Les Alignés[4]. Pia alikuwa mwanzilishi mwenza wa Collectif 212, kikundi cha wakurugenzi wa sanaa na wasanii kilicholenga kusaidia na kukuza sanaa ya kisasa kwa wasanii chipukizi nchini Morocco. Wanachama wa kikundi hicho walikuwa Hassan Echair, Safâa Erruas, Jamila Lamrani, Imad Mansour, Myriam Mihindou na Younés Rahmoun.[5]
Mwaka 1997, alimaliza makazi yake ya kwanza ya sanaa katika Hospitali ya Watoto huko Rabat, Morocco.Baadae, mwaka 2004, alikamilisha makazi yake ya pili ya sanaa katika Makumbusho ya Marrakech kupitia mpango wa ushirikiano wa Morocco na Ufaransa.Mwaka 2008, alihitimisha makazi yake ya tatu ya sanaa katika Castel de Denia, mji wa Denia nchini Hispania[6][7].
Kupitia uchoraji, sanaa ya maonesho ya vitu na upigaji picha, Benbouchta hutumia maarifa yake ya anthropolojia kutafakari vitu vya kila siku, utu wa binadamu na mazingira yake ya kitamaduni. Kipaumbele kikuu cha kazi zake ni kuunganisha masuala ya kijamii, hususan siasa za jinsia, ndani ya sanaa yake[8].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Amina Benbouchta - Biography, Shows, Articles & More". Artsy (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
- ↑ Amine, Khalid (2016-05). "After the 'Years of Lead' in Morocco: Performing the Memory". New Theatre Quarterly (kwa Kiingereza). 32 (2): 121–141. doi:10.1017/S0266464X16000038. ISSN 0266-464X.
{{cite journal}}: Check date values in:|date=(help) - ↑ "Sabrina Amrani Gallery - Artists | Amina Benbouchta". www.sabrinaamrani.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
- ↑ "BENBOUCHTA | METALOCUS". www.metalocus.es (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
- ↑ "Collectif 212". universes.art (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
- ↑ "Sabrina Amrani Gallery - Artists | Amina Benbouchta". www.sabrinaamrani.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
- ↑ "‘Down the rabbit hole’ by Amina Benbouchta". Islamic Arts Magazine (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
- ↑ "Amina Benbouchta - Biography, Shows, Articles & More". Artsy (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Amina Benbouchta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |