Amina Ahmed El-Imam
Amina Aahmed El-Imam (alizaliwa Julai 27, 1983) ni mwanabiolojia mwanamke wa kutokea nchini Nigeria, msomi na mwanasiasa mwenye nafasi ya kuwa Kamishna wa Afya ndani ya Jimbo la Kwara. Mahali alipozaliwa panaitwa Offa, Jimbo la Kwara na ni mhadhiri mkuu wa biolojia kwenye Chuo Kikuu cha Ilorin, Nigeria. [1] [2] [3]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa kwenye mnamo 27 Julai 1983, kwenye nchi yake Nigeria. El-Imam alifanikiwa kusoma shahada ya mikrobiolojia ndani ya Chuo Kikuu cha Ahmadu Bello, Zaria, Nigeria. [4] Alijiigiza kwenye ushirika wa miezi 9 kama Msomi Mgeni wa Fulbright kwenye Chuo Kikuu cha Jimbo la North Carolina, Raleigh, North Carolina.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]El-Imam, ni mhadhiri mkuu aliyejikita kwenye mikrobiolojia ya chakula na viwanda ndani ya Chuo Kikuu cha Ilorin, anafanya kazi kwa mshiriki wa kitivo kwenye mikrobiolojia. Alifanikiwa kuchukua Shahada yake ya Uzamivu katika Mifumo na Viumbe vya Kibiolojia dani ya Chuo Kikuu cha Nottingham ndani ya Uingereza mwaka wa 2017. Safari yake ya kitaaluma pia inajumuisha Shahada ya Uzamili kwenye fani hiyo hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Ahmadu Bello mwaka wa 2007 na shahada ya kwanza kwenye Mifumo na Viumbe vya Kibiolojia kutoka chuo kikuu hicho mwaka wa 2003.
Kielimu
[hariri | hariri chanzo]El-Imam ameshikilia nafasi ya mhadhiri mkuu wa mikrobiolojia dani ya Chuo Kikuu cha Ilorin, Nigeria, pamoja na kuwa mtaalamu wa mikrobiolojia ya chakula na viwanda. Utafiti wake umebobea kwa asilimia kubwa juu ya uhifadhi wa chakula na kuelewa vijidudu vinavyohusiana na kuharibika kwa vyakula mbalimbali vya kitamaduni. Anasimamia kundi la utafiti linajloikita katika uboreshaji wa takwimu wa michakato ya uchachushaji.
Siasa
[hariri | hariri chanzo]El-Imam alifanikiwa kupata nafasi ya Kamishna wa Afya wa Jimbo la Kwara kwenye tarehe ya Septemba 5, 2023 baada ya kuchaguliwa mwaka wa Julai 27, 2023 [5] na kupokea uthibitisho mwaka wa Agosti 29, 2023. [6]
Mafanikio yanayoonekana
[hariri | hariri chanzo]El-Imam aliunganika na Bodi ya Ushauri ya PressPayNg, Taasisi ya Teknolojia ya Elimu yenye kutoa suluhu za ufadhili wa ubunifu kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu ndani ya nchi ya Nigeria. [7] Ameandika vitabu viwili, "Kujua Vijidudu" na "Usimamizi wa Wakati kwa Wanawake Wataalamu," ambavyo vilizinduliwa siku yake ya kuzaliwa. [8]
Kuchaguliwa kwa El-Imam ulithibitishwa kwenye tarehe Agosti 29, 2023, kwa nafasi ya mkuu wa Wizara ya Afya ya Jimbo la Kwara, akiwa pamoja na cheo cha Kamishna wa Afya wa Jimbo la Kwara.
El-Imam ni mshirika wa Shirika la Wanawake kwenye Sayansi kwa Nchi Zinazoendelea. [9]
Huduma za Kimatibabu huko Kwara
[hariri | hariri chanzo]El-Imam, alikuwa mshiriki hai kwenye mipango tofauti tofauti. Hizi ni jumla ya programu za uhamasishaji wa kimatibabu kote jimboni, ziara ya Hospitali Maalum ya Offa, [10] na ziara rasmi kwa mwathiriwa wa mti ulioanguka huko Ilorin. Pamoja nahayo hayo, alishika jukumu la msingi kwenye kuadhimisha Kampeni ya Surua ya 2023 na Uhamasishaji wa Chanjo ya Kawaida huko Ilorin [11] Idhini ya Gavana ya uhamasishaji wa afya kote jimboni ilisisitiza zaidi umuhimu wa juhudi hizi. [12] Kwa ujumla yote, Dkt. El-Imam alifanikiwa kupata jukumu la Kituo cha Matibabu ya Saratani, [13] alikuwa na shughuli ya takwimu za kutisha za vifo 62,000 vya saratani kila mwaka ndani ya nchi ya Nigeria, kama ilivyoangaziwa na Gavana Abdulrahaman Abdulrazaq mwaka Oktoba 6, 2023. Mbinu hii pana inaonyesha kujitolea kwake katika kuboresha huduma ya afya na kushughulikia masuala muhimu ya afya katika Jimbo la Kwara.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Amina M. Ahmed El-Imam". scholar.google.com.my. Iliwekwa mnamo 2023-11-10.
- ↑ "Amina Ahmed El-Imam | University of Ilorin - Academia.edu". unilorin.academia.edu. Iliwekwa mnamo 2023-11-10.
- ↑ "You are being redirected..." kwarastate.gov.ng. Iliwekwa mnamo 2023-11-10.
- ↑ "Amina Ahmed El-Imam, Ph.D." ASM.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-11-10.
- ↑ Salami, Biodun (2023-08-18). "What do you know about Kwara female commissioner-nominee Dr Amina El-Imam?". Nigerian Sketch (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-11-10.
- ↑ "Commissioner-designate, Dr Amina Ahmed El-Imam, appreciates Gov. AbdulRazaq, Olofa, Speaker, APC leaders, others". Solid Media (kwa Kiingereza). 2023-08-29. Iliwekwa mnamo 2023-11-10.
- ↑ press_admin (2022-05-26). "Dr. Amina Ahmed El-Imam joins PressPayNg Advisory Board". PressPayNg Blog (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-11-10. Iliwekwa mnamo 2023-11-10.
- ↑ "Dr. Amina Ahmed El-Imam Archives". 21 Machi 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Ahmed El-Imam Amina". OWSD (kwa Kiingereza). 2018-09-05. Iliwekwa mnamo 2023-11-10.
- ↑ "FREE SURGICAL OUTREACH ENTERS 2ND WEEK". 2023-10-08. Iliwekwa mnamo 2023-11-10.
- ↑ "KWARA GOVT LAUNCHES ANTI-MEASLES VACCINATION CAMPAIGN FOR UNDER-FIVE CHILDREN" (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2023-10-28. Iliwekwa mnamo 2023-11-10.
- ↑ Fagbayi, Grace (2023-09-19). "Kwara free health sugry". Radio Kwara News (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-11-10. Iliwekwa mnamo 2023-11-10.
- ↑ Ogor, Jennifer (2023-10-06). "Kwara lays foundation for cancer treatment centre". FRCN HQ (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Novemba 2023. Iliwekwa mnamo 2023-11-10.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)