Nenda kwa yaliyomo

Amina Abubakar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Amina Abubakar ni Profesa Mshirika wa Saikolojia na Afya ya Umma kutokea nchini Kenya kwenye Chuo Kikuu cha Pwani. Yeye ni mwanachama wa utafiti kwenye Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kenya. Utafiti wake unatilia manani ucheleweshaji wa ukuaji kwa watoto wanaoumwa VVU, utapiamlo na malaria. Yeye ni mwanachama wa heshima kwenye Chuo Kikuu cha Oxford.

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Abubakar alitunukiwa Shahada ya Kwanza ya Elimu kwenye Chuo Kikuu cha Moi, baada ya hapo akasomea saikolojia ya elimu kwenye Chuo Kikuu cha Kenyatta . [1] Alikamilisha Shahada yake ya Uzamivu (PhD) kwenye Chuo Kikuu cha Tilburg mwaka wa 2008. Utafiti wake ulizingatia vitu vilivyochangia hatari na ustahimilivu kwa watoto wachanga ndani Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara . [2] Alikuwa mwanafunzi wa udaktari kwenye Chuo Kikuu cha Utrecht na Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu ya Kenya . [3] [4] [5]

Utafiti na kazi

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 2014 Abubakar aliungana na Chuo Kikuu cha Lancaster kama Mshiriki wa Marie Curie . [6] Anashikilia tuzo ya Baraza la Utafiti wa Kimatibabu la Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Viongozi wa Utafiti wa Afrika. Ametengeneza mikakati ya kugundua, kufuatilia na kurekebisha watoto walio kwenye hatari. [7] Alifanya utafiti wa jinsi mambo ya muktadha yanavyoathiri ustawi wa vijana zaidi ya 7,000 juu ya nchi 24. [8] [9] Amebaini hatua zilizofanikiwa kusaidia ukuaji wa kisaikolojia wa watoto wenye VVU Afrika Mashariki. [10] Aligundua kuwa hakuna uhusiano kati ya dalili za huzuni za akina mama na matokeo ya kiafya ya watoto wa Kiafrika.

Abubakar alichaguliwa kuwa profesa msaidizi kwenye Chuo Kikuu cha Pwani mwaka wa 2016. [11] Yeye ndiye msimamizi wa kundi la utafiti wa sayansi ya neva huko Kilifi . [12] Alikuwa mshindi wa Tuzo ya Royal Society Pfizer ya mwaka wa 2016. [13] Mwaka 2017 alichapisha Kitabu cha Mwongozo wa Sayansi ya Maendeleo Inayotumika katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara . [14] Kwenye kipindi hicho aliteuliwa kuwa Mwanachama wa Chuo cha Sayansi cha Afrika . [12]

  1. "Culture and Human Development". International Association for Cross-Cultural Psychology. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-29. Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  2. Abubakar, Amina; Van De Vijver, Fons J.R.; Mithwani, Sadik; Obiero, Elizabeth; Lewa, Naomi; Kenga, Simon; Katana, Khamis; Holding, Penny (Mei 2007). "Assessing Developmental Outcomes in Children from Kilifi, Kenya, Following Prophylaxis for Seizures in Cerebral Malaria". Journal of Health Psychology. 12 (3): 417–430. doi:10.1177/1359105307076230. ISSN 1359-1053. PMC 4825880. PMID 17439993.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Abubakar, Amina; Holding, Penny; Van de Vijver, Fons J.R.; Newton, Charles; Van Baar, Anneloes (2009-11-27). "Children at risk for developmental delay can be recognised by stunting, being underweight, ill health, little maternal schooling or high gravidity". Journal of Child Psychology and Psychiatry. 51 (6): 652–659. doi:10.1111/j.1469-7610.2009.02193.x. PMC 2919164. PMID 19951363.
  4. Abubakar, Amina; Holding, Penny; Van Baar, Anneloes; Newton, Charles R. J. C.; Van de Vijver, Fons J. R.; Espy, Kimberly Andrews (2013-09-04). "The Performance of Children Prenatally Exposed to HIV on the A-Not-B Task in Kilifi, Kenya: A Preliminary Study". International Journal of Environmental Research and Public Health. 10 (9): 4132–4142. doi:10.3390/ijerph10094132. PMC 3799506. PMID 24008985.
  5. "Handbook of African Educational Theories and Practices" (PDF). Human Development Resource Centre. Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  6. Safdar, Saba; Kosakowska-Berezecka, Natasza (2015-04-29). Psychology of gender through the lens of culture : theories and applications. Safdar, Saba F.,, Kosakowska-Berezecka, Natasza. Cham. uk. 408. ISBN 9783319140056. OCLC 908336077.{{cite book}}: CS1 maint: location missing publisher (link)
  7. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named ":0".
  8. Globally, Forum on Investing in Young Children; Board on Children, Youth; Health, Board on Global; Medicine, Institute of; Council, National Research (2014-08-18). Participant Biographies (kwa Kiingereza). National Academies Press (US).
  9. "Measurement Invariance of the Brief Multidimensional Student's Life Satisfaction Scale Among Adolescents and Emerging Adults Across 23 Cultural Contexts - Forskning - Aarhus Universitet" (kwa Kidenmaki). doi:10.1177/0734282915611284. Iliwekwa mnamo 2018-05-28. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)
  10. "Invited Speakers". www.issbd2014.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-06-12. Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  11. "Meet The Team | Neuro Development". neurodev.kemri-wellcome.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-29. Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  12. 1 2 "AAS Fellows in Kenya". African Academy of Sciences. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-13. Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  13. "2016 Royal Society Pfizer Award Seminar with Dr Amina Abubakar". royalsociety.org (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2018-05-28.
  14. Abubakar, Amina; Van De Vijver, Fons J.R (2017-11-17). Handbook of Applied Developmental Science in Sub-Saharan Africa. Abubakar, Amina,, Van de Vijver, Fons J. R. New York, NY. ISBN 9781493973286. OCLC 1017978244.{{cite book}}: CS1 maint: location missing publisher (link)