American Association of People with Disabilities
American Association of People with Disabilities (kifupi: AAPD; yaani Chama cha Watu wenye Ulemavu Marekani) ni shirika la Marekani lisilo na faida, ambalo hutetea haki za kisheria za watu wenye ulemavu, lenye makao makuu yake mjini Washington, D.C.[1]
Dhamira ya AAPD ni kuongeza nguvu ya kisiasa na kiuchumi kwa watu wenye ulemavu. Kama shirika la haki la Kitaifa linaloongozwa na watu wenye ulemavu mtambuka, AAPD inatetea haki za kiraia kikamilifu, ambapo ni zaidi ya Wamarekani millioni 60 wenye ulemavu. AAPD inahimiza fursa sawa; kiuchumi, uhuru wa kuishi na ushiriki kisiasa kwa watu wenye ulemavu.[2]
Moja ya malengo ya msingi ya AAPD ni kuhimiza zaidi utekelezaji wa Sheria ya Wamarekani wenye ulemavu.[1]
Historia
[hariri | hariri chanzo]AAPD ilianzishwa mnamo Julai 25, 1995 na Paul Hearne, Senator Bob Dole, John D. Kemp, Justin Dart, Tony Coelho, Pat Wright, Jim Weisman, Lex Frieden, Sylvia Walker, Paul Marchand, Fred Fay, I. King Jordan, Denise Figueroa, Judi Chamberlin, Bill Demby, Deborah Kaplan, Nancy Bloch, Max Starkloff, Mike Auberger, Neil Jacobson, Ralph Neas, Ron Hartley, na wengine.[3]
Shughuli zake
[hariri | hariri chanzo]AAPD inatetea kikamilifu haki za kiraia kwa Wamarekani wenye ulemavu. AAPD ina misingi minne ya sera na kanuni, ikiwa ni pamoja na; ushirikiano wa kijamii, fursa sawa katika uchumi wa kujitegemea, haki sawa na ushiriki wa kisiasa, na haki ya kupata huduma bora za kiafya. AAPD inatetea watu wenye ulemavu katika masuala mbalimbali ya kisera, ikijumuisha mada kama; ushirikiano wa kijamii, COVID-19, elimu, ajira, afya, makazi, masuala ya kimataifa, teknolojia, usafiri na masuala ya kihistoria.[4]
AAPD inawatetea wale wenye ulemavu kwa kuhakikisha kuwa wanapata makazi bora na salama. Inafanya kazi kwa kuhakikisha kuwa Sheria ya Haki ya Makazi, Sheria ya Ukarabati na Sheria ya Wamerekani wenye Ulemavu zinafuatwa.[5]
Ushiriki wa raia na upigaji kura
[hariri | hariri chanzo]Kampeni ya AAPD's REV UP (Jiandikishe, Elimisha, Piga kura, Tumia nguvu yako) inalenga kuongeza usajili wa wapiga kura kwa watu wenye ulemavu, kupambana na vizuizi na ukandamizaji unaojitokeza katika uchaguzi kwa wapiga kura, na kuelimisha wapiga kura katika masuala yanayoikabili jumuiya ya walemavu.[6] AAPD hufanya kazi kwa kushirikiana na shirika lisiloegemea upande wowote la VoteRiders[7] ili kueneza taarifa mahususi za serikali kuhusu mahitaji ya kitambulisho cha mpiga kura.Mradi wa Kura ya Walemavu
Mradi wa kura ya walemavu
[hariri | hariri chanzo]Uliongozwa na Jim Dickson, Makamu wa Rais wa zamani katika kuendeleza ushirikiano wa kiraia wa AAPD, ukijumuisha makundi 36 ya kitaifa yanayohusiana na ulemavu ambayo lengo lilikuwa ni kutoa ushiriki sawa wa kisiasa kwa wale wenye ulemavu. Malengo makuu ya mradi huo ni pamoja na mageuzi ya uchaguzi, kampeni za Get-Out-The-Vote, elimu ya wapiga kura na upatikanaji wa tovuti ya kupiga kura.[8]
Wiki ya haki ya kupiga kura kwa walemavu
[hariri | hariri chanzo]AAPD huwa inadaa wiki maalumu ya kupiga kura kwa ajili ya watu wenye ulemavu "Wiki ya Haki ya Kupiga kura kwa Walemavu (DVRW)" ambapo hufanyika kila Septemba ya mwaka. Ukurasa wa AAPD's DVRW unasema kwamba "Wiki ya Haki ya Kupiga Kura kwa Walemavu inahusu kulinda haki za watu wenye ulemavu ili washiriki kikamilifu." Shughuli za DVRW ni pamoja na kuandaa tukio la kusajili mwapiga kura au kuwaelinisha, kubadilishana nyenzo na rasilimali za upigaji kura na kuwaomba viongozi wa serikali za mitaa kuhusu kutangaza Wiki ya Haki ya Kupiga Kura kwa Walemavu.[9]
Wiki ya Haki ya Kupiga Kura kwa Walemavu hapo awali ilifahamika kama Wiki ya Kitaifa ya Usajili wa Wapiga Kura kwa Walemavu. AAPD ilifanya kwa mara ya kwanza Wiki ya Kitaifa ya Usajili wa Wapiga Kura kwa Walemavu mnamo 2016, kabla ya uchaguzi wa Urais wa Marekani wa 2016.[10]
Siku ya ushauri kwa walemavu
[hariri | hariri chanzo]Kufuatia tangazo la Rais Bill Clinton mnamo 1999, Siku ya Ushauri kwa Walemavu ilianzishwa ili kutoa nasaha na ushauri wa kazi kwa watu wenye ulemavu.[11][12] AAPD inasimamia programu ya Mwezi wa Kitaifa wa Ufahamu wa Ajira kwa Wamalemavu. Kila Oktoba ya mwaka, Siku ya Ushauri huadhimishwa kote nchini, huku zaidi ya vijana 10,000 wenye ulemavu wakishiriki katika shughuli zinazoungwa mkono na zaidi ya taasisi 1,500 za kibiashara, kihisani, za kiserikali na za kielimu.[13]
Fahirisi ya usawa wa walemavu
[hariri | hariri chanzo]Fahirisi ya Usawa wa Walemavu, iliwezeshwa kwa pamoja na AAPD na Disability:IN, ni desturi ya kila mwaka, kutambua ujumuishwaji wa walemavu katika nguvu kazi. Makampuni yana kategoria 6: utamaduni na uongozi, wigo mpana wa biashara, ajira kwa vitendo, ushirikiano wa kijamii na wasambazaji tofauti.[14]
Fursa
[hariri | hariri chanzo]Programu ya mafunzo kazini
[hariri | hariri chanzo]Ilianzishwa mnamo 2002, programu ya AAPD ya majira ya joto huwaleta pamoja wanafunzi wa chuo, wanafunzi waliohitimu, wanafunzi wa sheria na wahitimu wa hivi karibuni wenye ulemavu katika mafunzo ya kulipwa ya majira ya joto na makongamano ya ya kiofisi, mashirika ya shirikisho, mashirika yasiyo ya faida na yasiyo ya faida yanayopatikana ndani eneo la Washington DC.[15] Zaidi ya hayo, wahitimu wanalinganishwa na Mshauri katika ushiriki wa programu ya Cheti cha Utetezi wa Walemavu.
Mnamo 3 Machi 2003, AAPD ilitangaza kuanzishwa kwa programu ya AAPD Fall Internship kwa ufahili kutoka Arconic Foundation.[16] Programu ya Fall Internship huratibiwa kuanzia Oktoba hadi Desemba. Wanafunzi wanaomaliza mafunzo hukamilisha mafunzo yanayotolewa katika tovuti zilizochaguliwa awali. Kwa programu ya majira ya kiangazi, wahitimu wanalinganishwa na Mshauri katika ushiriki wa programu ya Cheti cha Utetezi wa Walemavu.[17]
Wahitimu wa mashuhuri wa programu ya mafunzo kazini ni pamoja na Lydia X. Z. Brown, Ari Ne'eman, Stacey Milbern na Leah Katz-Hernandez.[18][19][20]
Tuzo ya kiongozi ya Paul G. Hearne
[hariri | hariri chanzo]Paul G. Hearne ni mwanaharakati wa haki za walemavu, ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi wa Baraza la Kitaifa la Walemavu, alianzisha kwa mara ya kwanza ya huduma za kisheria kwa walemavu, iliyoelekezwa Just One Break Inc. kutoka 1979 mpaka 1989, na kuchagiza utayaarishaji wa rasmu ya kihistoria ya Sheria ya Wamarekani wenye Ulemavu ya 1990.[21] Kuanzishwa kwa tuzo ya kiongozi ya Paul G. Hearn, adhima ni kuwatambua viongozi wanaochipukia wenye ulemavu. Wapokeaji hupokea ufadhili ili kuanzisha au kuendeleza mradi mpya au uliopo ili kuongeza fursa kwa watu wenye ulemavu. Wapokeaji wa awali ni pamoja na Claudia L Gordon, Lauren Ridloff, Jerry White, Cheri Blauwet, Victor Pineda, Maureen McKinnon-Tucker, Anjali Forber-Pratt, Jason DaSilva, Alice Wong na Lydia X. Z. Brown.[22]
NBC Universal Tony Coehlo Media Scholarship
[hariri | hariri chanzo]Ufadhili huu ulipewa jina la Mwakilishi wa zamani wa Marekani na mfadhili wa awali wa Sheria ya Wamerekani wenye Ulemavu,Tony Coehlo, ufahili huu unafadhilia na NBCUniversal. Vigezo stahiki ni kwa wanafunzi wenye ulemavu ambao wanachukua taaluma katika tasnia za media, mawasiliano na burudani.[23]
Ushirika wa wasimuliaji wa haki za walemavu
[hariri | hariri chanzo]Ni msingi wa kusimamia haki, programu ya ushirika hutoa fursa kwa mtu binafsi na huwaleta pamoja watetezi wa walemavu kupitia masimulizi katika vyombo vya habari.[24]
Programu ya uongozi ya Fannie Lou Hamer
[hariri | hariri chanzo]Ilipewa jina la mwanaharakati wa haki za kiraia na kupiga kura kwa walemavu weusi, Fannie Lou Hamer ambaye alifanya kazi kama katibu mkuu wa SNCC, pia alichangia uundaji wa programu ya ustawi, na aliadhimia kupata shirikisho la bidhaa kwa ajili ya Waafrika wa Kimarekani.[25] Programu ya uongozi hutoa malipo kwa vijana weusi, watetezi wa walamavu ili kuunda kampeni za kitaifa zinazoongeza ushiriki na usajili wa wapiga kura.[26]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Home". AAPD (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-08-07.
- ↑ "About". AAPD (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-08-07.
- ↑ Imparato, Andrew J. 2005. "AAPD In Its Second Decade," AAPDnews (Spring 2005), p. 2.
- ↑ "Policy Principles". AAPD (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-08-07.
- ↑ "Housing". AAPD (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-03-04.
- ↑ Kigezo:Cite magazine
- ↑ VoteRiders Partner Organizations
- ↑ "Jim Dickson". fdrmemoriallegacy.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-03-05.
- ↑ "Disability Voting Rights Week". AAPD (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-08-07.
- ↑ Kigezo:Cite magazine
- ↑ "Supporting Americans With Disabilities". clintonwhitehouse4.archives.gov. Iliwekwa mnamo 2021-04-29.
- ↑ "Disability Mentoring Day | U.S. Department of Labor". www.dol.gov. Iliwekwa mnamo 2021-04-29.
- ↑ "Students get a glimpse of working world - Document - Gale In Context: Opposing Viewpoints". go.gale.com. Iliwekwa mnamo 2024-03-04.
- ↑ "Disability Equality Index". Disability:IN (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-22. Iliwekwa mnamo 2021-04-29.
- ↑ "AAPD Summer Internship Program". AAPD (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-04-29.
- ↑ "New Fall Internship Program from the American Association of People with Disabilities - AAPD", AAPD. (en-US)
- ↑ "Fall Internship Program". AAPD (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-08-07.
- ↑ "White House Highlights "Champions of Change"". abilitymagazine.com. Iliwekwa mnamo 2021-04-29.
- ↑ "Meet the Current Interns". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-12-20. Iliwekwa mnamo 2021-04-29.
- ↑ "In Her Own Words: Remembering and Honoring Stacey Park Milbern". Google Arts & Culture (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-19.
- ↑ "Paul G. Hearne, 48, Affable Champion of Disabled, Dies - Document - Gale In Context: Opposing Viewpoints". go.gale.com. Iliwekwa mnamo 2024-03-04.
- ↑ "Previous AAPD Paul G. Hearne Emerging Leader Award Recipients". AAPD (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-04-29.
- ↑ "NBCUniversal Tony Coelho Media Scholarship". AAPD (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-04-29.
- ↑ "Video Storytellers Program". Rooted in Rights (kwa American English). 19 Desemba 2022. Iliwekwa mnamo 2024-03-04.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hamlet, Janice D. (1996). "Fannie Lou Hamer: The Unquenchable Spirit of the Civil Rights Movement". Journal of Black Studies. 26 (5): 560–576. doi:10.1177/002193479602600503. ISSN 0021-9347. JSTOR 2784883. S2CID 144407724.
- ↑ "AAPD Announces the Launch of the Fannie Lou Hamer Leadership Program". AAPD (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-04-29.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |