Amerado (mwanamuziki)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Amerado
Amerado akiwa kwenye tuzo za 3Music Awards 2022
Amerado akiwa kwenye tuzo za 3Music Awards 2022
Alizaliwa 14 Februari 1995
Nchi Ghana
Kazi yake Rapa

Derrick Sarfo Kantanka, alizaliwa ( 14 Februari 1995 ), ni maarufu kwa jina la Amerado, ni rapa kutoka Kumasi . [1] [2] [3], na mtangazaji wa nchini Ghana .[4]

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Derrick Kantanka alizaliwa na kukulia huko Ejisu, Kumasi, katika Mkoa wa Ashanti nchini Ghana . Alisomea katika Shule ya upili ya KNUST . [5]

Kazi ya muziki[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kushika nafasi ya tatu katika Kipindi cha Solid FM Freestyle Show mwaka 2015, Amerado alikuja kumfahamu "Azee Ntwene", na kutia nae saini katika rekodi lebo yake ya MicBurnerz Music . [6] [7] Amerado alishirikishwa kwenye wimbo wa Mix Master Garzy ulionuiwa na kukuza amani kipindi cha uchaguzi mkuu wa Ghana wa mwaka 2016 . [8] Mwaka uliofuata, Amerado alitoa wimbo wake wa kwanza I AM, [9] ambao ulikua ni miongoni mwa nyimbo zao 10 bora nchini Ghana mnamo Januari 2017. [10] Alitoa EP yake ya kwanza ya Rapmare mnamo Novemba. [11] Mwaka 2018, Amerado alishirikishwa kwenye wimbo wa hip-hop wa Sarkodie "Biibi Ba", [12] [13] ambao uliteuliwa kwa Wimbo Bora wa Hiphop katika tuzo za muziki za Vodafone Ghana mwaka 2019 (Vodafone Ghana Music Awards). [14]

Mtindo[hariri | hariri chanzo]

Amerado hurap na kuimba zaidi katika lahaja ya Kitwi ya lugha ya Akan ya Ghana, lakini wakati mwingine hutumia Kiingereza pia. Jina lake la usanii, Amerado, ambalo linamaanisha 'Gavana' kwa Kiakan, lilichaguliwa ili kuthibitisha uongozi wake katika eneo la muziki. [15] [16]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Kumasi based musicians are not united – Amerado. www.ghanaweb.com (30 January 2019). Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-07-20. Iliwekwa mnamo 2019-05-19.
 2. Music (2018-01-31). Amerado; lyrical genius from Kumasi. Ghana Music. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-12-30. Iliwekwa mnamo 2018-12-07.
 3. Coronavirus has contributed to my popularity - Musician Amerado confesses (en-US). MyJoyOnline.com (2020-07-21). Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-07-21. Iliwekwa mnamo 2020-07-21.
 4. https://www.biographyweb.org/artists/amerado/
 5. ProfileAbility (2017-11-21). ProfileAbility – Amerado. ProfileAbility. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-12-09. Iliwekwa mnamo 2018-12-07.
 6. DaGhBlogger. Strongman Is The Best Rapper In Ghana And Amerado Is The Best In Kumasi—Azee Burner. Modern Ghana. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-14. Iliwekwa mnamo 2018-12-07.
 7. Stop the insults – Amerado cautions on 'Death Sentence'. BusinessGhana. Iliwekwa mnamo 2021-08-31.
 8. Mix Masta Garzy launches peace campaign | Music 2016-10-05. www.ghanaweb.com (5 October 2016). Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-12-30. Iliwekwa mnamo 2018-12-07.
 9. Mawuli (2017-01-19). New Music: Amerado - I Am (Prod. by Azee Burner). Pulse. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-07-14. Iliwekwa mnamo 2018-12-07.
 10. Top 10 Ghanaian songs of January 2017. Pulse (2017-02-02). Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-01-06. Iliwekwa mnamo 2019-01-06.
 11. Hundreds of fans attend Amerado's Rapmare EP launch | Entertainment 2017-11-27. www.ghanaweb.com (27 November 2017). Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-06-14. Iliwekwa mnamo 2018-12-07.
 12. Sarkodie picks 10 underground rappers to feature on 'Biibi Ba'. GhKings (2018-09-20). Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-04-08. Iliwekwa mnamo 2019-05-19.
 13. All You Need To Know About Sarkodie's "Biibi Ba" Challenge. Modern Ghana (2018-09-25). Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-04-08. Iliwekwa mnamo 2019-05-19.
 14. Full list of nominations for VGMA 2019. www.graphic.com.gh. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-04-08. Iliwekwa mnamo 2019-05-19.
 15. Quist (2020-07-12). My girlfriend left me because I was broke - Amerado Burner on past relationship (en). Yen.com.gh - Ghana news.. Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-06-26. Iliwekwa mnamo 2021-06-26.
 16. What does amerado mean?. www.definitions.net. Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-06-26. Iliwekwa mnamo 2021-06-26.
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amerado (mwanamuziki) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.