Nenda kwa yaliyomo

Amanya Mushega

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tarehe ya kuzaliwa27 Juni 1946
Mahali pa kuzaliwaBushenyi, Uganda
TaifaMganda
ElimuUDSM (LL.B)
Queen's University at Kingston (LL.M)
KaziMwanasheria, Mwanasiasa
WadhifaKatibu Mkuu wa 2 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Aprili 2001 – Aprili 2006)
MtanguliziFrancis Muthaura
MrithiJuma Mwapachu

Nuwe Amanya Mushega (anajulikana zaidi kama Amanya Mushega (alizaliwa katika Wilaya ya Bushenyi, Mkoa wa Magharibi wa Uganda, 28 Juni 1946) ni mwanasheria, mwanasiasa, dplomati, na mhudumu wa umma kutoka Uganda. Alihudumu kama Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuanzia 2001 hadi 2006.

Mushega alipata elimu yake ya awali nchini Uganda. Alihudhuria Shule ya Upili ya Mbarara kuanzia 1963 hadi 1966, kabla ya kuhamia Kings College Budo mwaka 1967. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1969 kusoma sheria. Alipata Shahada ya Sheria mwaka 1972 na baadaye alipata Shahada ya Uzamili ya Sheria kutoka Queen's University at Kingston|Queen's University mjini Kingston, Ontario, Kanada mwaka 1974. Mwishoni mwa miaka ya 1970, Mushega alijiunga na programu ya Daktari wa Falsafa katika London School of Economics lakini aliiacha aliposhiriki katika Harakati ya Upinzani wa Kitaifa (National Resistance Movement) mwaka 1981.[1]

Uzoefu wa kazi

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alirudi Uganda mwaka 1972 na kufundisha kama mwalimu msaidizi katika kitivo cha sheria cha Chuo Kikuu cha Makerere. Baada ya kupata shahada yake ya uzamili mwaka 1974, alihudumu kama mwalimu katika kitivo cha sheria cha Chuo Kikuu cha Zambia mjini Lusaka. Alirudi Chuo Kikuu cha Makerere mwaka 1979 kama mwalimu na kuendelea katika nafasi hiyo hadi mwaka 1981.

  1. |width="40%" style="text-align: center;" rowspan="1"|Secretary General of the East African Community
    April 2001 – 4 April 2006
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amanya Mushega kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.