Amani (mwanamuziki)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Cecilia Wairimu (alizaliwa mnamo 1980 mjini Thika), anafahamika zaidi kwa jina lake la jukwaa Amani, ni mwanamuziki wa pop kutoka Kenya.

Ameshinda tuzo mbalimbali, ikiwemo tuzo la mwanamke mwanamuziki bora katika tuzo za MAMA (MTV Africa Music Awards) mwaka wa 2009.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Alisomea katika shule ya Upili ya Bishop Gatimu Ngandu, ambako alikuwa katika kundi la accapella la Sobriety . Amani saini mkataba wa Ogopa Deejays mwaka wa 1999, punde tu alipomaliza skuli ya upili. Nyimbo yake ya kwanza "Move on" ilienea sana katika stesheni za redio na ilifuatwa na nyimbo zingine kama vile "Tahidi" na "Papii". Ushirikiano wake na Nameless mwaka wa 2002 katika nyimbo, 'Ninanoki', pia ilienea sana Nyimbo zake za baadaye zinajumuisha "Talk to You" (ikiwashirikisha Patonee na Big Pin), "Bad Boy" (ikimshirikisha Nyashinski wa Kleptomaniax), Usiwe Mbali (ikimshirikisha AY), "Tamani", "Missing My Baby" na "Tonight"

Albamu yake ya kwanza, Amani ilitolewa mwaka wa 2006 na kufuatiwa na Tamani . Ametembelea nchi ya Marekani na nchi nyinginezo

Tuzo / Kuchaguliwa[hariri | hariri chanzo]

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

 • Tuzo za muziki ya Kisima mwaka wa 2006 - sanii mwanadada wa mwaka [1]
 • Tuzo za muziki ya Kisima mwaka wa 2006 - ushirikiano wa mwaka( "Bad Boy" na Nyashiski) [1]
 • 2006 Tuzo za CHAT - Msanii maarufu mwanadada [2]
 • 2006 Tuzo za CHAT - nyimbo maarufu [2]
 • 2006 Tuzo za CHAT - Ushirikiano maarufu [2]
 • Tuzo za muziki ya Kisima 2007 - mwandada boomba [3]
 • 2007 Tuzo za muziki za lulu la Afrika (tuzo za PAM) - Msanii bora (Kenya) [4]
 • 2009 MTV Africa Music Awards - Msanii bora mwandada [5]

Kuchaguliwa[hariri | hariri chanzo]

 • 2002 Tuzo za CHAT [2]
 • 2006 Tuzo za muziki za lulu la Afrika - Msanii mwanadada bora wa Kenya[6]
 • Tuzo za muziki za Tanzania 2007 - Nyimbo bora katika Afrika ta Mashariki ( "Bad Boy") [7]
 • Tuzo za muziki za Tanzania 2007 - Nyimbo bora katika Afrika ta Mashariki ( "Missingmy Baby") [8]
 • 2008 Tuzo za video za muziki za Channel - video bora ya R & B barani Afrika( "Missing My Baby") [9]
 • 2008 Tuzo za video za muziki za Channel O - Nyimbo bora ya Afrika Mashiriki ( "Missing My Baby") [9]
 • 2009 Tuzo za video za muziki za Channel O - Nyimbo bora ya mwanadada ( "Tonight") [10]
 • 2009 Tuzo za video za muziki za Channel O - Video bora ya R & B video( "Tonight") [10]
 • 2009 Tuzo za video za muziki za Channel O - Bora Afrika Mashariki ( "Tonight") [10]
 • 2009 Tuzo za video za muziki za Channel O - Video ya mwaka( "Tonight") [10]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]