Amal Clooney
| Amal Clooney | |
|---|---|
Clooney mnamo mwaka 2022 | |
| Amezaliwa | Amal Alamuddin 3 Februari 1978 |
| Uraia | Uingereza, Lebanon, Ufaransa |
| Miaka ya kazi | 2000–hadi sasa |
| Mwenza | George Clooney (m. Error: Invalid time.–present) |
| Watoto | 2 |
Amal Clooney (jina la kuzaliwa Alamuddin; alizaliwa 3 Februari 1978)[1] ni mwanasheria wa kimataifa wa haki za binadamu mwenye asili ya Lebanon na Uingereza.[2][3] Amewahi kuwawakilisha wateja mbalimbali mashuhuri, wakiwemo rais wa zamani wa Maldivi Mohamed Nasheed,[4] mwanzilishi wa WikiLeaks Julian Assange,[5] waziri mkuu wa zamani wa Ukraine Yulia Tymoshenko,[6] mwanaharakati wa haki za binadamu wa Yazidi Nadia Murad,[7] mwandishi wa habari Mfilipino-Mmarekani Maria Ressa,[8] mwandishi wa habari wa Azerbaijan Khadija Ismayilova,[9] na mwandishi wa habari wa Misri-Canada Mohamed Fahmy.[10]
Clooney ni profesa wa sheria ya kimataifa katika Shule ya Serikali ya Blavatnik (Blavatnik School of Government) katika Chuo Kikuu cha Oxford[11] na mshirika mwandamizi katika Taasisi ya Teknolojia na Haki ya Oxford (Oxford Institute of Technology and Justice), taasisi aliyoanzisha kwa ushirikiano ili kutumia nguvu ya akili mnemba (AI) katika kuongeza fursa za upatikanaji wa haki.[12]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Amal Alamuddin alizaliwa huko Beirut, Lebanon, mnamo tarehe 3 Februari 1978.[13] Baba yake ni wa asili ya Wadruze wa Lebanon na mama yake ni Mwislamu wa dhehebu la Sunni kutoka Tripoli.[14] Alipokuwa na umri wa miaka miwili, familia yake ilihamia nchini Uingereza ili kukimbia Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe vya Lebanon, na walikaa huko Gerrards Cross katika jimbo la Buckinghamshire.[15] Ana ndugu watatu: dada mmoja (Tala Alamuddin) na kaka wawili wa kambo waliozaliwa kwenye ndoa ya kwanza ya baba yake.[16].
Clooney alisoma katika Shule ya Sekondari ya Dr Challoner (Dr Challoner's High School), shule ya wasichana ya mchepuo wa sarufi iliyopo Little Chalfont, Buckinghamshire. Baadaye alisoma katika Chuo cha St Hugh cha Oxford (St Hugh's College, Oxford), ambapo alitunukiwa ufadhili wa masomo na Tuzo ya Shrigley.[17][18][19] Mnamo mwaka 2000, alihitimu shahada ya kwanza ya sheria yenye hadhi ya daraja la pili la juu na kwa sasa ni mwanachama wa heshima wa chuo hicho cha St Hugh.[20][21]
Baada ya hapo, alijiunga na Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha New York (New York University School of Law) kwa ajili ya masomo ya Shahada ya Uzamili ya Sheria (LLM). Alipata Tuzo ya Ukumbusho ya Jack J. Katz kwa umahiri wake katika sheria ya burudani.[22][23] Alipokuwa chuoni hapo, alifanya kazi kwa muhula mmoja katika ofisi ya mwanasheria na jaji wa Marekani Sonia Sotomayor, ambaye wakati huo alikuwa jaji wa Mahakama ya Rufani ya Marekani kwa Mzunguko wa Pili na mmoja wa wakufunzi wa sheria wa NYU.[24]
Kazi ya sheria
[hariri | hariri chanzo]
Clooney ana sifa na vibali vya kufanya kazi ya sheria katika jimbo la New York pamoja na nchi za Uingereza na Wales. Alisajiliwa katika Chama cha Mawakili cha New York mnamo mwaka 2002.[4] Mnamo mwaka 2010, alitambuliwa rasmi kama wakili nchini Uingereza na Wales kupitia taasisi ya Inner Temple. Ni wakili anayefanya kazi katika chemba za Doughty Street Chambers.[4][25][26] Pia amewahi kufanya uwakili katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) huko The Hague.[22] Alifanya kazi katika kampuni ya sheria ya Sullivan & Cromwell jijini New York kwa miaka mitatu chini ya Kundi la Utetezi wa Jinai na Uchunguzi, ambapo baadhi ya wateja wake walikuwa makampuni ya Enron na Arthur Andersen.[19][22] Mnamo mwaka 2024, Clooney alitunukiwa tuzo ya mwanasheria bora wa mwaka ya Legal 500 kwa kutambua kazi na mchango wake mkubwa katika nyanja ya sheria za kimataifa.[27]
Clooney alihitimu mafunzo ya ukatibu wa kisheria wa jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki mnamo mwaka 2004, akifanya kazi chini ya majaji Vladlen S. Vereshchetin kutoka Urusi, Nabil Elaraby kutoka Misri,[28][29] na jaji wa dharura Franklin Berman kutoka Uingereza. Baadaye alihamia The Hague kufanya kazi katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya zamani ya Yugoslavia,[30] ambapo alikuwa msaidizi wa kisheria wa jaji mkuu Patrick Robinson. Kesi hiyo ilikuwa inamkabili Slobodan Milosevic, rais wa zamani wa Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia, aliyetuhumiwa kwa makosa ya jinai yaliyotendeka huko Kosovo, Croatia, na Bosnia wakati wa vita vya zamani vya Yugoslavia.[4] Clooney pia alifanya kazi kama mwendesha mashtaka katika Mahakama Maalum ya Lebanon. Aliongoza kesi dhidi ya wanachama watano wa kundi la Hezbollah, waliositakiwa kwa kuhusika na mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafic Hariri na watu wengine mnamo mwaka 2005.[31]
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]
Clooney ana uraia wa nchi za Uingereza, Lebanon,[32][33][34] na Ufaransa.[35] Anazungumza kwa ufasaha lugha ya Kiingereza na Kifaransa, na pia ana uwezo wa kuzungumza Kiarabu cha Lebanon.[4][36]
Mnamo tarehe 28 Aprili 2014, alichumbiwa na mwigizaji wa Marekani George Clooney,[37] ambaye walikutana kwa mara ya kwanza kupitia rafiki yao wa pamoja mnamo Julai 2013.[38] Mnamo tarehe 7 Agosti 2014, wawili hao walipata leseni ya ndoa katika Manispaa ya Kifalme ya Kensington na Chelsea (Royal Borough of Kensington and Chelsea) jijini London.[39] Siku mbili baada ya sherehe yao kubwa ya harusi,[40][41][42][43] walifunga ndoa rasmi mnamo tarehe 27 Septemba 2014 huko Ca' Farsetti katika jiji la Venice;[41][44][45][46] walifungishwa ndoa na rafiki wa karibu wa Clooney, Walter Veltroni, mwanasiasa wa Italia aliyewahi kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Italia kati ya mwaka 1996 na 1998 pamoja na kuwa Meya wa Roma kati ya mwaka 2001 na 2008.[43][47] Mnamo Oktoba 2014, ilitangazwa kuwa familia hiyo ya Clooney ilikuwa imenunua jumba la Mill House lililopo kwenye kisiwa cha Mto Thames huko Sonning Eye[48] kwa gharama ya takriban pauni milioni 10.[49]
Mnamo Februari 2017, kipindi cha televisheni cha Marekani cha The Talk kiliripoti kuwa Clooney alikuwa na ujauzito.[50] Mwigizaji wa Marekani Matt Damon, ambaye ni rafiki wa karibu wa familia hiyo, alithibitisha ujauzito huo kupitia kipindi cha Entertainment Tonight muda mfupi baadaye.[51] Mnamo Juni 2017, Clooney alijifungua watoto pacha wasiofanana, yaani: msichana na mvulana.[52]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Russian, Ale (5 Februari 2018). "Amal's Big 40! George Clooney Celebrates Wife's Birthday on 24-Hour Getaway". People. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Juni 2023. Iliwekwa mnamo 5 Februari 2018.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Amal Clooney Speaks About the Lebanese Protests". MTV Lebanon (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-12-22.
Amal Alamuddin Clooney, a Lebanese-British barrister and wife of famous actor Georges Clooney, expressed on Tuesday her love for Lebanon and her happiness with the Lebanese people standing in the face of the ruling regime.
- ↑ "George Clooney Finally Meets His Match With Human Rights Lawyer Amal Alamuddin". Vanity Fair. 29 Machi 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Septemba 2020. Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2019.
{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 4 5 "Amal Clooney". Doughty Street Chambers. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Rothman, Michael (19 Machi 2014). "5 Things About Amal Alamuddin". ABC News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Aprili 2014. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2014.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Johnston, Ian (27 Aprili 2014). "George Clooney Engaged To Amal Alamuddin: Actor To Marry British Human Rights Lawyer Who Has Represented Julian Assange". The Independent. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Aprili 2014.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Day, Emma (11 Desemba 2018). "Nadia Murad is Joined by Amal Clooney as She Accepts Nobel Peace Prize". Vogue Arabia.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Clooney, Amal (Juni 12, 2020). "Amal Clooney: A test for democracy in the Philippines". The Washington Post. Iliwekwa mnamo Desemba 26, 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Azerbaijan court frees journalist backed by Amal Clooney". BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2016-05-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Desemba 2023. Iliwekwa mnamo 2024-01-16.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kingsley, Patrick (6 Novemba 2014). "Amal Clooney calls on Egypt to release journalist Mohamed Fahmy". The Guardian. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Juni 2017. Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2019.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Amal Clooney appointed Visiting Professor of Practice at Blavatnik School of Government | University of Oxford". www.ox.ac.uk (kwa Kiingereza). 2025-02-06. Iliwekwa mnamo 2025-06-11.
- ↑ "People". www.techandjustice.bsg.ox.ac.uk (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-27.
- ↑ Rosenthal, Franz (2014). Gutas, Dimitri (mhr.). Man Versus Society in Medieval Islam. Leiden; Boston: Brill. uk. 613. ISBN 978-9-004-27089-3. OCLC 892338528.
- ↑ Pathbreakers of Arab America—Amal Alamuddin Clooney
- ↑ Flanagan, Padraic (28 Aprili 2014). "George Clooney Engaged to High-Flying British Lawyer". The Daily Telegraph. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Januari 2022.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Lebanon in frenzy over Clooney-Alamuddin engagement". NOW News. AFP. 1 Mei 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Oktoba 2014. Iliwekwa mnamo 28 Septemba 2014.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Savino, Christine (11 Julai 2025). "Amal Clooney recognised in British Vogue's 25 Most Influential Women". The Oxford Student. Iliwekwa mnamo 14 Februari 2026.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Colleges, Halls, and Societies: Notices – St Hugh's College". Oxford University Gazette. 23 Oktoba 1997. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Julai 2010. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2014.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 McNeal, Gregory S. (27 Aprili 2014). "International Lawyer And Scholar Amal Alamuddin Engaged To George Clooney". Forbes. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Septemba 2017. Iliwekwa mnamo 15 Septemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Profile - Amal Alamuddin - BBC Sounds". BBC (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-12-24.
- ↑ "Amal Clooney". St Hugh's College (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo 2023-12-29.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 "Amal Alamuddin". Doughty Street Chambers. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 31 Julai 2015. Iliwekwa mnamo 14 Mei 2015.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Schumann, Rebecka (29 Oktoba 2013). "George Clooney Girlfriend Revealed: Who Is Amal Alamuddin? 6 Fast Facts About The Actor's New Love". International Business Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Mathis-Lilley, Ben (28 Aprili 2014). "London Human Rights Lawyer Amal Alamuddin Is Engaged". Slate. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Januari 2018. Iliwekwa mnamo 28 Septemba 2014.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Gannaway, Atticus (Septemba 10, 2024). "Barrister Without Borders". NYU Law magazine.
{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ BSB. "Barrister Details – Mrs Amal Clooney". www.barstandardsboard.org.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Nicholas Bowen KC, Laura Dubinsky KC and Amal Clooney win awards at The Legal 500 Bar Awards Ceremony 2024 | Doughty Street Chambers". www.doughtystreet.co.uk (kwa Kiingereza). 2024-09-26. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Novemba 2024. Iliwekwa mnamo 2024-11-11.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Clerkships – Prior and Present Clerks". Institute for International Law and Justice. New York University School of Law. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Septemba 2014. Iliwekwa mnamo 28 Septemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Chi, Paul (27 Februari 2014). "George Clooney Engaged to Amal Alamuddin: 5 Fast Facts About Her". People. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Aprili 2017. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Alamuddin, A.; Webb, P. (2010). "Expanding Jurisdiction over War Crimes under Article 8 of the ICC Statute". Journal of International Criminal Justice. 8 (5): 1219. doi:10.1093/jicj/mqq066.
- ↑ "The Special Tribunal for Lebanon". global.oup.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Mei 2024. Iliwekwa mnamo 2024-05-21.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Orfanides, Effie (2025-05-01). "George Clooney Receives Major News Amid Concerns About His Wife". Yahoo!. Iliwekwa mnamo 2025-12-22.
Born in Lebanon, she holds duel citizenship in her birth country as well as Britain.
- ↑ Swoyer, Alex (2025-05-07). "Amal Clooney, wife of actor George Clooney, could be denied reentry to the U.S. over ICC warrants". The Washington Times (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-12-22.
Ms. Clooney, a British Lebanese international human rights lawyer, has not become a U.S. citizen since marrying Mr. Clooney in 2014.
- ↑ Miller, Mike (7 Juni 2017). "With American George and British Amal, What's Next for the Clooney Twins?". People. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Novemba 2022. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2022.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "George Clooney et sa family obtiennent la nationalité française par naturalisation" [George Clooney and his family obtain French nationality by naturalisation]. Le Monde (kwa Kifaransa). 2025-12-29. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-12-30. Iliwekwa mnamo 2025-12-29.
- ↑ Respers France, Lisa (28 Aprili 2014). "What we know about George Clooney's fiancée". CNN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Mei 2014. Iliwekwa mnamo 13 Mei 2014.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Cohen, Sandy (28 Aprili 2014). "George Clooney sheds most eligible bachelor status, gives up serial romance for engagement". Star Tribune. Associated Press. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Aprili 2014. Iliwekwa mnamo 13 Mei 2014.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Gonzales, Erica (31 Januari 2018). "George Clooney First Met Amal in the Comfort of His Own Home". Harper's Bazaar. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Julai 2019. Iliwekwa mnamo 4 Julai 2019.
{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Rothman, Michael (7 Agosti 2014). "George Clooney and Fiancée Amal Alamuddin Get Marriage License". ABC News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Agosti 2014. Iliwekwa mnamo 27 Juni 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Anderson, Ariston (15 Septemba 2014). "George Clooney Wedding Details Leaked by Italian Media". The Hollywood Reporter. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Septemba 2014. Iliwekwa mnamo 27 Septemba 2014.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 Kington, Tom (27 Septemba 2014). "Clooney And Bride Appear in Public After Wedding". Sky News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 27 Novemba 2014.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Oldenburg, Ann; Puente, Maria (27 Septemba 2014). "George Clooney, Amal Alamuddin marry in Venice". USA Today. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 24 Agosti 2017.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 Fornasier, Claudia (15 Septemba 2014). "George, sì davanti a Veltroni". Corriere della Sera. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Oktoba 2014. Iliwekwa mnamo 27 Septemba 2014.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Inside George Clooney and Amal Alamuddin's Wedding". People. 5 Oktoba 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Oktoba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "George Clooney and Amal Alamuddin's wedding". CBS News. 26 Septemba 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Desemba 2014. Iliwekwa mnamo 13 Januari 2015.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Squires, Nick (29 Septemba 2014). "George Clooney's wedding to Amal Alamuddin finally ends". The Daily Telegraph. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Januari 2022.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Squires, Nick (15 Septemba 2014). "George Clooney 'to be married by ex-Rome mayor'". The Daily Telegraph. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Januari 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Sawer, Patrick (10 Oktoba 2014). "Welcome to Sonning, Mr & Mrs Clooney". The Daily Telegraph. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Januari 2022.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Sawer, Patrick (9 Oktoba 2014). "George Clooney snaps up £10 million manor house in Sonning, Berkshire". The Daily Telegraph. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Januari 2022.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "George and Amal Clooney 'expecting twins'". BBC News. 10 Februari 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Februari 2017. Iliwekwa mnamo 21 Juni 2018.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Rothman, Michael (10 Februari 2017). "Matt Damon Says George and Amal Clooney Will Be 'Great Parents'". ABC News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo 27 Juni 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Leonard, Elizabeth; Juneau, Jen (6 Juni 2017). "A Boy! A Girl! George and Amal Clooney Welcome Twins". People. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Juni 2017. Iliwekwa mnamo 6 Juni 2017.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
