Nenda kwa yaliyomo

Amadou Sagna

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Amadou Sagna (alizaliwa tarehe 10 Juni, 1999) ni mchezaji wa kulipwa wa Senegal wa soka anayekipiga kama mshambuliaji wa klabu ya Ufaransa En Avant Guingamp.

Kazi ya klabu

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 9 Julai 2019, Sagna alisaini mkataba na timu ya Ligi Kuu ya Daraja la Kwanza ya Ubelgiji ya Club Brugge KV.[1][2]

Mnamo 22 Agosti, 2020, Sagna alicheza mechi yake ya kwanza ya kitaaluma akiwa na Club NXT, timu ya akiba ya Club Brugge, katika Ligi Daraja la Kwanza B ya Ubelgiji. Alianza kikosi cha kwanza na kucheza kwa dakika 85 dhidi ya RWDM47, huku NXT wakishindwa kwa mabao 0–2.

Mnamo 26 Mei, 2022, Club Brugge ilitangaza kuwa Sagna alikuwa amesaini mkataba wa kudumu na klabu ya Ligue 2, Chamois Niortais F.C. (Niort).

Mnamo 6 Julai, 2023]], Sagna alisaini mkataba wa miaka mitatu na En Avant Guingamp (Guingamp).

Kazi ya kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 13 Mei, 2019, ilitangazwa kuwa Sagna angekuwa sehemu ya kikosi cha mwisho cha Senegal kwa Kombe la Dunia la FIFA la U-20 la mwaka 2019.[3]

  1. Adewoye, Gbenga (9 Julai 2019). "Senegal's Amadou Sagna joins Club Brugge". Goal.com. Iliwekwa mnamo 18 Oktoba 2020.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Sagna joins Oostende on loan". Club Brugge (Twitter).
  3. Profile at the Club Brugge website
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amadou Sagna kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.