Nenda kwa yaliyomo

Alphonce Simbu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alphonce Felix Simbu
Simbu kwenye Marathoni ya London 2017
Tarehe ya kuzaliwa14 Februari 1992
TaifaMtanzania
KaziMwanariadha (mbio ndefu)
MichezoRiadha
Tukio kuuMarathoni
Uzito55 kg
Rekodi binafsi2:04:38 (Marathon)
MedaliDhahabu – Mashindano ya Dunia ya 2025 Tokyo (Marathon)

Shaba – Mashindano ya Dunia ya 2017 London (Marathoni)
Fedha – Michezo ya Jumuiya ya Madola 2022 Birmingham (Marathon)

Dhahabu – Boston Marathon 2025 (Marathon)

Alphonce Felix Simbu (alizaliwa Mampando, kata ya Ntuntu, wilaya ya Ikungi, mkoa wa Singida, 14 Februari 1992) ni mwanariadha wa mbio ndefu wa Tanzania aliyejikita zaidi katika mbio za marathoni.[1] Ni bingwa wa dunia kwenye mbio za marathoni, baada ya kushinda mbio za Mashindano ya Dunia ya Riadha ya mwaka 2025, na kuwa mwanariadha Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mashindano ya kidunia, baada ya kukimbia kilomita 42.195 kwa saa 2:09:48. [2][3][4]

Kazi ya Michezo

[hariri | hariri chanzo]

Simbu alishiriki katika mbio za marathoni kwenye Mashindano ya Dunia ya Riadha mwaka 2015 yaliyofanyika Beijing, China.

Mwaka 2016, Simbu aliiwakilisha Tanzania katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Kiangazi katika mbio za marathon kwa wanaume. Alimaliza nafasi ya tano kwa muda wa saa 2:11:15. Pia alibeba bendera ya Tanzania katika sherehe ya kufunga michezo hiyo.[5][6]

Simbu alishinda toleo la 14 la Marathoni ya Mumbai tarehe 15 Januari 2017.[7] Mwaka huohuo alishinda medali ya shaba katika Marathoni ya Mashindano ya Dunia ya Riadha 2017 kwa muda wa saa 2:09:51

Mwaka 2019, Simbu alishiriki tena katika mbio za marathon za wanaume kwenye Mashindano ya Dunia ya Riadha yaliyofanyika Doha, Qatar, akamaliza katika nafasi ya 16.[8] He finished in 16th place.[8]

Mnamo Juni 2021, Simbu alifuzu kuiwakilisha Tanzania kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya 2020 (iliyocheleweshwa), ambapo alimaliza nafasi ya 7 kwa muda wa saa 2:11:35.[9]

Simbu alishinda medali ya fedha katika Michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka 2022 kwenye mbio za marathoni kwa wanaume.[10]

Mwezi Desemba 2024, Simbu alimaliza nafasi ya 4 katika Marathoni ya Valencia na kuweka rekodi yake binafsi ya saa 2:04:38.[11]

Mwaka 2025, Simbu alimaliza nafasi ya pili katika Marathoni ya Boston kwa muda wa saa 2:05:04.[12]

  1. http://www.iaaf.org/athletes/tanzania/alphonce-felix-simbu-287379 |title=Alphonce Felix Simbu |publisher=IAAF |date=22 August 2015| accessdate=22 August 2015
  2. https://www.mwananchi.co.tz/mw/michezo/simbu-aandika-historia-duniani-akiipa-tanzania-dhahabu-5193378
  3. "Alphonce Felix Simbu". IAAF. 22 Agosti 2015. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Simbu takes Tanzania's first global title with marathon victory in Tokyo". World Athletics.org. Iliwekwa mnamo 15 Septemba 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Rio 2016". Rio 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2016. Iliwekwa mnamo 24 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "The Flagbearers for the Rio 2016 Closing Ceremony". 21 Agosti 2016. Iliwekwa mnamo 24 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Simbu sizzles: Tanzanian overcomes stiff challenge from second-placed Kipkorir to win elite full marathon - Latest News & Updates at Daily News & Analysis". 16 Januari 2017. Iliwekwa mnamo 16 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. 1 2 "Marathon Men − Final − Results" (PDF). IAAF. 5 Oktoba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 27 Juni 2020. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Only three athletes to represent Tanzania at Tokyo Olympic games". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 20 Juni 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Marathon - Men's Marathon". BBC Sport. Iliwekwa mnamo 30 Julai 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. Final Results
  12. Schad, Tom (Aprili 21, 2025). "Boston Marathon 2025 live: Race updates, highlights, results of 129th running". usatoday.com. Iliwekwa mnamo Aprili 21, 2025.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)