Alifa Rifaat
| Fatimah Rifaat | |
![]() | |
| Amezaliwa | 5 Juni 1930 Misri |
|---|---|
| Amekufa | Januari 1996 |
| Nchi | Misri |
| Majina mengine | Alifa Rifaat |
| Kazi yake | Mwandishi |
Fatimah Rifaat (alizaliwa Juni 5 1930 ,alifariki Januari 1996), alijulikana Kama Alifa Rifaat (Kiarabu: أليفة رفعت), alikua mwandishi wa nchini Misri ambaye hadithi zake fupi zenye utata zilijulikana wakati wa maonyesho ya mienendo ya mahusiano ,jinsia ya kike na katika utamaduni wa Misri.[1] Wakati wakichukua mada kama hizi zenye utata, wahusika wakuu wa Fatimah Rifaat walibaki waaminifu kidini na hisia za kupita kiasi kuelekea hatima yao. Hadithi zake hazikujaribu kudhoofisha mfumo dume; bali zilitumiwa kuonyesha matatizo yaliyomo katika jamii ya wahenga wakati wanaume hawazingatii mafundisho yao ya kidini ambayo yanawapasa kuwatendea wemawanawake. Fatimah Rifaat alitumia jina bandia la Alifa ili kuzuia aibu kwa upande wa familia yake kutokana na mandharia ya hadithi zake na kazi yake ya uandishi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Alifa Rifaat's 91st Birthday". Google. 5 Juni 2021.
