Alice Nkom
Alice Nkom (alizaliwa 14 Januari 1945) ni wakili, mwanasiasa na mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Kamerun. Anajulikana zaidi kwa kutetea haki za watu wa LGBTQ+ nchini. Alice Nkom anatajwa kuwa mwanamke wa kwanza katika Afrika ya Kati kuwa wakili. Pia amekuwa akipigania kuondolewa kwa sheria zinazofanya ushoga kuwa kosa la jinai katika eneo hilo.
Nkom alianza kusoma sheria katika Toulouse School of Law katika Chuo Kikuu cha Toulouse Capitole nchini Ufaransa. Baadaye alimalizia masomo yake katika University of Yaoundé nchini Cameroon. Tangu mwaka 1969, amekuwa akifanya kazi ya uwakili katika mji wa Douala, Cameroon. Alipokuwa na umri wa miaka 24, alikua mwanamke wa kwanza mweusi anayezungumza Kifaransa kupokelewa rasmi kuwa mwanasheria nchini Cameroon.
Msimamo wa Kisiasa na Matukio ya Hivi Karibuni
[hariri | hariri chanzo]Mwezi Machi 2020, Paul Atanga Nji, ambaye alikuwa Waziri wa Utawala wa Kimaeneo nchini Cameroon, aliishutumu taasisi ya REDHAC iliyokuwa ikiongozwa na Alice Nkom. Pia aliishutumu mashirika kama Human Rights Watch, Amnesty International na International Crisis Group kwa kile alichokiita kuwa ni “njama” dhidi ya Cameroon na vyombo vya usalama vya nchi hiyo. Tarehe 6 Desemba 2024, serikali ilipiga marufuku REDHAC pamoja na mashirika mengine ya kutetea haki za kiraia. Serikali ilisema sababu ilikuwa ni wasiwasi kuhusu namna mashirika hayo yalivyokuwa yakitumia fedha.Tarehe 10 Desemba 2024, Alice Nkom aliitwa na polisi kwa ajili ya mahojiano baada ya kuvunja muhuri uliowekwa kwenye milango ya ofisi za REDHAC mjini Douala. Hakuenda kwenye mahojiano hayo wala kwenye miito iliyofuata. Aliomba mahojiano hayo yaahirishwe hadi Januari 2025 ili aweze kuhakikisha kuwa wakili wake anakuwepo. Tarehe 18 Desemba 2024, katika kusikilizwa kwa kesi katika mahakama ya kijeshi, Nkom alishutumiwa kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia makundi yenye silaha katika maeneo yanayozungumza Kiingereza nchini Cameroon. Tarehe 31 Desemba 2024, aliitwa tena kwa mahojiano na kitengo cha uchunguzi wa makosa ya jinai cha jeshi la polisi la taifa.Tarehe 9 Januari 2025, Amnesty International ilitoa wito kwa mamlaka za Cameroon kuondoa kusimamishwa kwa mashirika hayo, kuyarejeshea haki ya kufanya kazi na kuyaacha kufanya shughuli zao bila kuingiliwa kiholela. Pia ilitaka matumizi ya mfumo wa haki kusitishwe katika kuwashambulia Alice Nkom na watetezi wengine wa haki za binadamu.Rais
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Alice Nkom kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |