Nenda kwa yaliyomo

Alice Cooper

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alice Cooper
AmezaliwaVincent Damon Furnier

Februari 4, 1948 (Miaka 78)

Detroit, Michigan, Marekani
Kazi yakeMuimbaji na mtunzi wa nyimbo
Miaka ya kazi1964–sasa
MwenzaSheryl Goddard (kuoana 1976)
Watoto3, akiwemo Calico Cooper

Alice Cooper (alizaliwa Vincent Damon Furnier; 4 Februari 1948)[1] ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo wa Marekani. Katika kazi yake iliyodumu kwa miongo sita, anajulikana kwa sauti yake ya mikwaruzo na maonyesho ya jukwaani ya uigizaji yanayohusisha vifaa vingi vya maigizo na michezo ya kiini macho. Cooper anachukuliwa na waandishi wa habari za muziki pamoja na wasanii wenzake kama 'Baba wa Muziki wa Shock Rock' (The Godfather of Shock Rock).[2] Ametumia vionjo kutoka kwenye filamu za kutisha, sanaa ya uigizaji ya vaudeville, na muziki wa garage rock ili kuanzisha mtindo wa muziki wa rock wa kutisha na wa kiigizaji uliokusudiwa kuwashtua watazamaji.[3][4]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Vincent Damon Furnier alizaliwa mnamo Februari 4, 1948, huko Detroit, Michigan, akiwa mtoto wa kiume wa Ether Moroni Furnier (1924–1987) na mke wake Ella Mae (jina la utotoni McCart; 1925–2022). Alipewa jina hilo kwa heshima ya mjomba wake, Vincent Collier Furnier, na mwandishi wa hadithi fupi Damon Runyon.[5][6]

  1. ↑ https://www.nme.com/artists/alice-cooper
  2. ↑ https://www.washingtonpost.com/entertainment/music/how-concerts-shifted-from-songs-to-spectacles/2014/05/22/ca521340-d6ce-11e3-8a78-8fe50322a72c_story.html
  3. ↑ https://www.allthingsloud.com/alice-cooper-still-godfather-shock-rock/
  4. ↑ https://www.allmusic.com/artist/alice-cooper-mn0000005953
  5. ↑ https://books.google.co.tz/books?id=1I-lN2IAo_wC&pg=PA9&redir_esc=y
  6. ↑ https://www.azcentral.com/story/entertainment/music/2015/06/06/alice-cooper-band-interviews-history/28625657/
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alice Cooper kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.