Ali bin Said wa Zanzibar
Mandhari

Sayyid Ali bin Said al-Busaidi, GCSI (takriban 1854 – 5 Machi 1893) alikuwa Sultani wa nne wa Zanzibar. Alitawala Zanzibar kuanzia tarehe 13 Februari 1890 hadi 5 Machi 1893. Mnamo Juni 1890, alilazimika kukubali Zanzibar kuwa chini ya ulinzi wa Uingereza (British Protectorate) katika makubaliano rasmi kati yake na Mwakilishi Mkuu wa Serikali ya Uingereza.[1]
Baada ya kifo chake, alirithiwa na mpwa wake, Hamad bin Thuwaini Al-Busaid.
Heshima
[hariri | hariri chanzo]- Knight Kamanda Mkuu wa Agizo la Nyota ya India (GCSI) – 1890
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Provisional agreement concluded between the Sultan of Zanzibar and Her Britannic Majesty's Agent and Consul General, respecting the British Protectorate of the Sultan's dominions, 14th June, 1890. Map of Africa by Treaty, Vol. I. (British Colonies, Protectorates and Possessions in Africa, via archive.org)
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ali bin Said wa Zanzibar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |