Nenda kwa yaliyomo

Alexander Pistohlkors

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Alexander Erichovich von Pistohlkors (6 Juni 1885 mjini Saint Petersburg – 8 Septemba 1941 mjini Brest, France) alikuwa afisa wa Kikosi cha Ulinzi cha Kifalme cha Urusi (Russian Imperial Guard) aliyejulikana kwa ukatili wake katika kuzima uasi kufuatia Mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1905.[1]

Chimbuko na uhusiano

[hariri | hariri chanzo]

Pistohlkors alizaliwa katika familia ya kikabaila ya Pistohlkors yenye asili ya Kifini [Kigezo:Separated entries].[2] Alikuwa mtoto wa Olga Valerianovna Karnovich na mume wake wa kwanza, Meja Jenerali Erich Gerhard Augustinovich von Pistohlkors (1853–1935), ambaye alipeana naye talaka kabla ya ndoa yake ya pili mnamo mwaka 1902.

Kupitia ndoa ya pili ya mama yake na Grand Duke Paul Alexandrovich wa Urusi, alikuwa kaka wa kambo wa Grand Duke Dmitri Pavlovich wa Urusi, mmoja wa waliopanga njama za kumuua Grigori Rasputin. Dada yake mdogo, Marianne, naye pia anasemekana kuwa miongoni mwa waliopanga njama hizo za mauaji.[3]

  1. Radzinsky, Edvard, The Rasputin File, Doubleday, p. 218
  2. Markkanen-Vänttinen, Mira (31 Mei 2023). "Laura Netzel, Pistolekors Pyyvilän kartanosta". Rantasalmen Lehti (kwa Kifini). Iliwekwa mnamo 25 Oktoba 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Radzinsky, pp. 476-477
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alexander Pistohlkors kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.